Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Sunday, July 1, 2018

Jaji mkuu ataka madalali wasimamiwe vyema

adv1
JAJI Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Juma amewakumbusha viongozi wa Mahakama kusimamia kwa makini upangaji na utendaji wa madalali ili kudhibiti matumizi mabaya ya fedha za wadaiwa.

Alisema hayo jijini Dodoma jana wakati akikabidhi hati 24 za uteuzi kwa Mahakimu Wafawidhi wa Mikoa pamoja na kushuhudia uapisho wa Naibu Wasajili tisa uliofanywa na Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Dk Eliezer Feleshi. Profesa Juma alisema kuwa mara nyingi shughuli za madalali hulalamikiwa, wananchi wanafahamu kuwa madalali ni sehemu ya Mahakama, kwa hiyo eneo hilo lazima liangaliwe kwa umakini hasa pale fedha za wadaiwa zinapotumiwa vibaya na baadhi ya madalali.

“Pamoja na Kanuni za sasa kuwataka madalali wapitie mafunzo lakini bado mna wajibu wa kusimamia majukumu yao, pia tunazifanyia mabadiliko kanuni za madalali ambapo watalazimika kuweka fedha zote kwenye akaunti ya Mahakama kabla ya kuweka katika akaunti zao ili tuweze kudhibiti matumizi mabaya ya fedha ambazo ni dhamana kwa wananchi,” alisema.

Profesa Juma aliongeza kuwa upangaji wa kesi ni eneo lingine linalotakiwa kusimamiwa kwa umakini kwani kesi zinatakiwa zipangwe kwa kuzingatia muda wa kusajiliwa au vipaumbele maalumu kama maelekezo yanavyotolewa na viongozi wa Mahakama hali itakayosaidia kuepusha malalamiko kutoka kwa wananchi.

Aidha, aliwataka viongozi hao kuwa kichocheo cha maboresho ya Mahakama ya Tanzania pamoja na kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu mkubwa na bila upendeleo wowote huku wakizingatia sheria, kanuni na miongozo mbalimbali iliyowekwa. Vile vile aliwakumbusha kuwa uteuzi wao ni ishara tosha kwamba wameaminiwa kutekeleza majukumu yaliyoainishwa katika ngazi hizo za uteuzi na wameshakuwa walezi wa watumishi katika maeneo yao hivyo ni jukumu lao kuwatambua viongozi wa baadaye ambao watachukua nafasi zao.

Akizungumzia kuhusu mfumo wa kisasa wa kielektroniki katika utoaji wa huduma, Profesa Juma alisema kuwa mfumo huo wa kufungua mashauri kwa njia ya kielektroniki utasimamiwa na Msajili Mkuu ambapo vitaanzishwa vibanda vya kuwasaidia wananchi kufungua mashauri kwa kielektroniki lengo likiwa ni kumaliza kabisa tatizo la upoteaji wa majalada.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )