Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Tuesday, July 24, 2018

JWTZ Kuadhimisha Siku Ya Mashujaa Kwa Kufanya Shughuli Za Kijamii

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limesema kesho July 25 litatoa huduma kwa kufanya shughuli mbalimbali za kijamii kufuatia kumbukumbu  ya siku ya Mashujaa waliopoteza uhai wakipigania Taifa.

Msemaji Mkuu wa JWTZ Makao makuu, Kanali Ramadhani Dogoli amesema kuwa Jeshi hilo (NGOME) watatoa huduma ya vipimo vya Shinikizo la Damu, Kisukari, Uchunguzi wa Kinywa na Meno ushauri nasaha na kupima VVU kwa hiari pamoja na kufanya usafi viwanja vya Mnazi mmoja ambavyo vitatumika kufanyia vipimo hivyo.

Aidha, amesema Kamandi ya Vikosi chini ya Makao Makuu vitashiriki usafi katika maeneo mbalimbali yakiwemo Hospitali ya Temeke, Zakhiem, Dar Group na masoko ya Mbagala, Temeke, Tandika.

Pia amesema vikosi hivyo vitafanya shughuli za upandaji miti katika shule ya Wailes na stendi ya mabasi ya Mbagala na Temeke.

Kwa upande wa Zanzibar Brigedia ya Nyuko watashiriki usafi katika masoko ya Mombasa, Sebuleni Majumba ya Wazee na Mwanakwerekwe.

Shughuli zote zitatembelewa na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )