Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Wednesday, July 4, 2018

Kangi Lugola Kaanza na Sakata la Lugumi

adv1
Waziri wa Mambo ya Ndani, Mh. Kangi Lugola ameweka wazi kwamba tayari amekwishampa taarifa Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Simon Sirro kumuandalia taarifa muhimu kuhusiana na suala la Lugumi.

Mh. Lugola ametoa kauli hiyo akiwa mkoani Mbeya ikiwa ni siku mbili tu zimepita tangu ale kiapo cha kuwa Waziri katika Wizara hiyo na kupokea maagizo hayo kama sehemu muhimu ya kuanzia kazi yake.

Kangi amesema kwamba amemuagiza Mkuu wa Polisi Simon Sirro kumuandalia taarifa itakayompa muongozo kushughulika na suala la Lugumi jambo ambalo Rais Magufuli amekuwa akitaka kupatiwa majibu haraka iwezekanavyo.

Aidha, Mh. Lugola amesema ingawa yeye siyo mgeni sana katika suala sakata hilo la Lugumi kwa kuwa jambo ameshalisikia mara kadhaa ndani ya bunge, ila sasa hivi anataka kulifuatilia jambo hilo kiofisi zaidi kuliko bungeni.

"Leo nimeanza na Mbeya, nimemuagiza Sirro juu ya kuniandalia taarifa itakayoniondolea ugeni katika suala la Lugumi. Lugumi siyo ngeni sana kwangu kwa kuwa mimi ni Mbunger na jmabo hili lilishakuja bungeni. Nataka kushughulika nayo kiosisi. Nikirudi Dar esa salaam sasa ndio nitadili na yale maagizo mengine kwa hiyo nao wanapaswa kukaa mkao" Lugola.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )