Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Thursday, July 5, 2018

Kauli ya Magufuli yaliamsha Jeshi la Polisi

Ikiwa ni siku chache tangu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli kutoa maagizo kwa viongozi kuwajibika na wasisubiri hadi mwenyewe awawajibishe na kutolea mfano wa ajali zilizofuatana jijini Mbeya.

Alfajiri ya leo Julai 5, 2018, Kikosi cha Polisi Usalama Barabarani Kanda Maalum Dar es salaam kimezindua Operesheni ya Ukaguzi wa magari, madereva, leseni na vyeti vya udereva kwa madereva wa mabasi ya Mikoani katika stendi kuu ya Ubungo .

Zoezi hilo limeongozwa na Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Liberatus Sabas, ambapo amesema kuwa lengo la operesheni hiyo ni kuwafanya madereva  kuacha tabia ya kughushi leseni, kuwahimiza wajiunge na mafunzo ya udereva katika vyuo vinavyotambulika na serikali.

“Polisi Kanda Maalum Dar es salaam inawataka Madereva wasio na leseni halali, madereva walevi, pamoja wamilki wa magari walio na magari mabovu kutoyaruhusu  magari hayo kuingia barabarani hadi yatakapotengenezwa na kukaguliwa”, amesema Kaimu Kamanda.

Kamanda ameongeza kuwa Jeshi la Polisi halitasita kuchukua hatua kali za kisheria kwa wamiliki, Madereva na Kampuni za usafirishaji zitakazoenda kinyume na sheria, kanuni na taratibu za usalama
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )