Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Friday, July 6, 2018

Magari Mabovu Marufuku Dodoma

Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani jijini Dodoma limewaonya wamiliki wa magari mabovu kutoyaingiza  barabarani hadi hapo watakapoyafanyia matengenezo.

Akizungumza leo Julai 6, 2018 katika mafunzo ya wanahabari kuhusu usalama barabarani, kaimu mkuu wa usalama barabarani Mkoa wa Dodoma,  ASP Swaleh Digega amesema mpaka sasa zaidi ya magari mabovu 30 yamekamatwa.

Ametaja aina ya magari yanayoshikiliwa mpaka sasa kuwa ni pamoja na yale yanayobeba mchanga, magari madogo na yanayobeba abiria.

Amesema uchakavu wa magari husababisha foleni zisizo na msingi, kwamba yanaongeza ajali za barabarani kwa kuwa mengi hufeli breki.

"Gari ukilitembelea ikifika muda fulani unalifanyia matengenezo, tunaposema gari kuu kuu tunamaanisha ni yale yenye matatizo, yasiyo na breki, chakavu, namba yake inaning’inia. Taa hakuna, mengine hayawaki mpaka yasukumwe,” amesema.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )