Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Sunday, July 1, 2018

Mahakama yazindua mfumo mpya kuendesha mashauri

adv1
MAHAKAMA ya Tanzania imezindua mfumo wa uendeshaji mashauri kwa kutumia magari ‘mobile court’ katika maeneo yasiyofi kika na kwenye mikusanyiko ya watu na kesi mbalimbali zikiwemo za madai ya chini ya Sh milioni 100. Kwa kuanzia, mahakama mbili zinazohama zinatarajiwa kuanza kutoa huduma baadaye mwaka huu.

Zinatengenezwa Afrika Kusini ambapo moja inatarajiwa kukamilika Julai na nyingine Septemba. 

Mahakama imesema, ina mpango wa kuongeza mahakama hizo zinazohamishika ziwe sita iwapo zitapokelewa vema watakaposhughulikia migogoro na mashauri ya madai yasiyozidi Sh milioni 100. 

Mfano wa mahakama hiyo uko katika viwanja vya Mwalimu Nyerere vilivyopo barabara ya Kilwa, Dar es Salaam yanapofanyika maonesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa (DITF) maarufu kama Sabasaba yanayoendelea hadi Julai 13, mwaka huu.

Akizungumza katika maonesho hayo, Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Ufuatiliaji na tathmini wa mahakama, Sebastian Lacha alisema magari hayo yatakuwa na mfumo wa uendeshaji mahakama yenye uwezo wa kukaa watu wanne akiwemo karani, mwendesha mashtaka na hakimu. Alisema wananchi na wadau watakuwa na sehemu ya kukaa nje ya mahakama hiyo itakayoendeshwa maeneo yaliyochaguliwa masoko au kwa wafugaji.

Mkurugenzi Msaidizi wa mahakama, Daniel Msangi alisema mchakato wa kubadilisha sheria ili kutambua mahakama zinazotembea uko katika hatua za mwisho kabla ya kuanza utekelezaji. 

Alisema kuanzia Septemba wataanza kutoa elimu kwa wananchi jinsi ya kufungua mashauri na sehemu za kufungulia na kutoa huduma kwa majaribio kwa mwaka mmoja jijini Dar es Salaam.

Alisema kama huduma itapokelewa vyema na wananchi, watanunua magari mengine sita na kusambaza maeneo mbalimbali ikiwemo yasiyofi kika kwa urahisi kama visiwani na kwa wafugaji wakiangalia kuwa na mahakama za boti. 

Alisema gharama ya kutengeneza mahakama moja yenye vifaa vyote ikiwemo intaneti na mifumo ya kimahakama ni takribani Sh milioni 300 hadi 350. Alisema uendeshaji kesi utakuwa ule wa kawaida.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )