Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Sunday, July 1, 2018

Majadiliano gesi asilia kubeba maslahi ya taifa

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema serikali inachukua tahadhari kwenye majadiliano ya utekelezaji wa mradi wa Kuchakata na Kusindika Gesi Asilia (LNG) utakaogharimu dola za Marekani bilioni 30. Majaliwa aliyasema hayo alipokuwa akilihutubia bunge wakati wa kuahirisha Mkutano wa 11 wa Bunge mjini hapa.

Alisema kutokana na umuhimu wa mradi huo kwa taifa, serikali imekuwa makini katika majadiliano hayo na kampuni za kimataifa za mafuta katika utekeleza mradi huo. 

“Ni vema tukatambua kuwa mradi huu una maslahi makubwa kwa taifa, hivyo Serikali inachukua tahadhari kubwa kwenye majadiliano yanayoendelea baina ya Timu ya Majadiliano ya Serikali (GNT) na kampuni za mafuta (IOCs)... serikali inaendelea na majadiliano na kampuni hizi ili mradi huo uanze kutekelezwa mapema kwa kuzingatia maslahi mapana ya nchi yetu,” alisema.

Serikali kupitia Shirika la Maendelo ya Petroli Tanzania (TPDC) inatarajia kutekeleza mradi huo kwa kushirikiana na wawekezaji ambao ni kampuni za kimataifa za mafuta ikiwa ni hatua ya kuendeleza rasilimali hiyo. 

Mjaliwa alisema mradi huo ambao utatumia gesi asilia iliyogunduliwa kwenye kina kirefu cha bahari, una lengo la kuiwezesha Tanzania kuvuna na kuuza rasilimali ya gesi katika soko la dunia sambamba na kukidhi mahitaji ya soko la ndani yanayojumuisha matumizi ya viwanda na majumbani.

Alisema mradi huo ambao unachukua eneo lenye ukubwa wa hekari 2,071.7 pamoja na mambo mengi utasaidia kuongeza mapato ya serikali kupitia mauzo ya gesi katika soko la ndani na nje. 

“Pia itasaidia upatikanaji wa nishati ya uhakika kwa ajili ya viwanda na matumizi ya nyumbani na pia kuwa chanzo cha malighafi za viwanda kwa ajili kuzalisha mbolea, plastiki na kimikali za petrol,” alisema.

Alisema mradi huo pia utakuwa chanzo cha ajira ambapo wakati wa ujenzi wake, mradi huo utaajiri takribani watu 10,000 na wengine wapatao 3,000 wakati wa uendeshaji. 

Majaliwa alisema pia utasaidia ukuaji wa uchumi wa miji la Lindi na Mtwara utakaokwenda sambamba na kupanuliwa kwa bandari na uwanja wa ndege.
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )