Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Wednesday, July 4, 2018

Mbeya waanza kutekeleza agizo la Rais Magufuli

Siku moja baada ya Rais John Magufuli kuagiza hatua zichukuliwe kudhibiti ajali mkoani Mbeya, kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa huo imekutana kwa dharura kwa ajili ya utekelezaji wa agizo hilo na kufikia maazimio sita ambayo yatasaidia kudhibiti ajali mkoani humo, ikiwemo kuimarisha ukaguzi wa magari na kufufua barabara ya zamani ya Mbalizi kama njia mbadala ya kupunguza madhara ya mtelemko mkali wa Mbalizi.

Katika kikao hicho cha dharura chenye lengo la kutekeleza agizo la rais Magufuli, kamati hiyo ikiwa chini ya uenyekiti wa mkuu wa mkoa wa Mbeya Amos Makalla imefikia maazimio sita yenye lengo la kukabiliana na ajali mkoani Mbeya.

Maazimio mengine ya kamati hiyo ni pamoja na kuwaondoa wafanyabiashara wote walio kwenye hifadhi za barabara kwa madai kuwa wako kwenye hatari ya kupata ajali, kuwekwa kwa alama za barabarani kwenye maeneo yote zinapohitajika, ajenda ya usalama barabarani kuwa ya kudumu kwenye kamati za ulinzi za wilaya na kurekebisha miundombinu ya barabara katika maeneo yote hatarishi
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )