Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Friday, July 6, 2018

Mganga aliyedai ana dawa ya kuzuia risasi, apigwa risasi afariki

Mganga mmoja nchini Nigeria amefariki baada ya mteja wake kujaribu iwapo ana nguvu za kuzuia risasi kuingia mwilini mwake kama alivyodai.

Chinaka Adoezuwe, 26, aliuawa baada ya kumuagiza mteja wake kumpiga risasi alipokuwa akivaa nguvu hizo za kuzuia risasi katika shingo yake.

Maafisa wa polisi katika jimbo lililopo kusini mashariki la Imo wanasema kuwa mteja huyo sasa amekamatwa kwa kosa la mauaji.

Nguvu za uganga ni maarufu nchini Nigeria , ambapo waganga huombwa kuwatibu raia magonjwa tofauti.

Ili kuthibitisha kwamba nguvu hizo zinafanya kazi , alisimama na kumpatia mteja wake bunduki ili aweze kuthibitisha dawa hiyo na hapo ndipo janga hilo likatokea!.

Mnamo mwezi Januari , muuzaji wa dawa za kienyeji alikamatwa baada ya mtu mmoja aliyedaiwa kunywa maji ya kuzuia risasi kuuawa.

Chanzo: Bbc swahili

Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )