Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Saturday, July 28, 2018

Mrema Aridhishwa na Utendaji Kazi wa Kangi Lugola....Adai kwa Kasi Hiyo Ataweza Kuvaa Viatu vyake

Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Labour Party (TLP), Augustine Mrema amesema ameridhishwa na utendaji kazi wa Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola huku akidai akiendelea kufanya hivyo ataweza kukivaa kiatu chake cha uwaziri wa Mambo ya Ndani enzi ya kipindi chake cha mwaka 1990.

Mrema ametoa kauli hiyo jana Julai 27, 2018 wakati alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari kwenye makao makuu ya chama hicho kilichopo Magomeni jijini Dar es Salaam na kusema Rais Magufuli amepata Waziri mzuri ambaye ataweza kusafisha nchi kama ataweza kuendelea na mwendo alikuwa nao sasa.

"Bila ya kuwa na kiongozi imara nchi inayumba, lakini Rais Magufuli kampata Waziri wa Mambo ya Ndani Kangi Lugola anayefanya vizuri na ninaweza nikasema akiendelea hivi ataweza kuvivaa viatu vyangu kwasababu Wizara ya Mambo ya Ndani ndio kioo na taa. Uchafu wowote ambao unataka kuondoshwa kwenye nchi lazima Wizara ya Mambo ya Ndani ishughulike nao...

"Jinsi Waziri Lugola alivyoanza kazi yake mimi amenitia moyo na kuwatia moyo watanzania wengi kwamba sasa tunaweza kuisafisha nchi hii. Ili lengo la Rais wetu lifikiwe la kujenga nchi yenye amani, haki pamoja na watu wanaobambikiza wenzao kesi lazima wachukuliwe hatua", alisema Mrema

Pamoja na hayo Mrema aliendelea kwa kusema "tunaye Rais Dkt. John Magufuli ambaye analeta mapinduzi makubwa katika nchi yetu, anafanya kazi kubwa sana hivyo ni lazima alindwe kwa gharama yoyote. Mimi nimekuwa kiongozi katika nchi hii sijapata kuona mfano wa Rais jasiri, mwenye uthubutu wa kufanya yale mambo ambayo yameshindikana yaliyokuwa yakitutisha sisi".

Mnamo mwaka 1990, Augustine Mrema aliteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani hadi mwaka 1994 ambapo alibadilishwa Wizara hiyo na kuhamishiwa katika Wizara ya Kazi, Maendeleo ya Vijana na Michezo.

Julai 19, 2018, Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola alibaini upotevu wa mbwa wa Polisi anayejulikana kwa jina la 'hobby' wakati alipokuwa kwenye ziara yake katika Kikosi cha Farasi na Mbwa kilichopo eneo la Bandari Jijini Dar es Salaam na kumuagiza IGP Sirro kutoa maelezo ya upotevu wa mbwa.

Pamoja na hayo, Waziri Lugola ameshamtaka IGP Simon Sirro amtafute mmiliki wa kampuni ya Lugumi popote pale alipo na kumfikisha ofisini kwake Julai 31 saa mbili asubuhi ili ajue hatma yake ikiwa ile ya kudaiwa kuwepo na ufisadi.

Mbali na hilo Waziri Lugola pia amemuagiza Mkurugenzi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) afike ofisini kwake Julai 25 akiwa na waliopewa tenda ya kuleta mtambo wa kutengeneza vitambulisho vya taifa ili kwenda kumueleza kwani mtambo huo haujaletwa au waende na pesa walizopewa na Serikali.

Waziri Lugola tayari ameshatoa matamko mengi na sasa ikiwa ni wiki ya tatu tangu alipoapishwa, kwa mujibu wake amesema anajitahidi kufanyia kazi maagizo yote aliyopatiwa wakati anaapishwa na kama Waziri ni wajibu wake kutafuta matokeo chanya ya haraka ili Rais aweze kupumzika na kuwatumikia wananchi kwenye maendeleo
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )