Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Thursday, July 5, 2018

Msigwa: Sifikirii kuwa Rais, lakini 2020 Chadema tunachukua nchi

Mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msigwa amesema kuwa uchaguzi ujao wa mwaka 2020 anaamini kuwa chama chake kitakwenda kushinda kwa kishindo kikubwa.

Amesema kuwa CHADEMA imejipanga na ushindani wa mwaka 2020 katika uchaguzi mkuu ambapo amesema kuwa imani yake ni kuchukua dola.

Aidha, amesema wananchi wameona ni kwa kiasi gani walivyodanganywa na namna ahadi nyingi zilizotolewa zimeshindwa kutekelezwa hivyo anaamini kwamba hawataweza kufanya kosa la kuirudisha CCM madarakani.

“Ushindi wa Chadema 2020 utakuwa ni wa kishindo sana. Wananchi wamejionea kila mahali wanalia maisha magumu, yamekuwa ni mwiba kwao, na ushindi wetu utakuwa na kasi ya kimbunga,”amesema Msigwa

Hata hivyo, akizungumzia kuhusu suala la yeye kufikiria kuwa Rais siku moja kupitia chama chake, amesema kuwa bado hajapata maono hayo.
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )