Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Thursday, July 26, 2018

Mtoto Wa Miaka Miwili Afanyiwa Ukatili Wa Kulawitiwa Na Kaka Yake Wilayani Ukerewe.

Mtoto wa miaka miwili mkazi wa kijiji cha Ihebo Kata ya Muriti Wilayani Ukerewe mkoani Mwanza, amekumbwa na tukio la ukatili wa kijinsia baada ya kulawitiwa na kaka yake (mtoto wa baba yake mkubwa) aliyefahamika kwa jina la ese benaya, miaka 19.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Naibu Kamishina wa Polisi Ahmed Msangi amesema tukio hilo limetokea jana majira ya saa sita mchana.

“Tarehe 25.07.2018 majira ya saa 12:00  mchana, Mtoto mdogo mwenye umri wa miaka miwili jina tunalihifadhi, mkazi wa kijiji cha Ihebo, alilawitiwa na kaka yake aliyefahamika kwa jina la Ese Benaya, miaka 19, mkazi kijiji cha ihebo na kumsababishia maumivu makali katika sehemu zake za siri, kisha baada ya kufanya ukatili huo mtuhumiwa alitoroka kusiko julikana, kitendo ambacho ni kosa kisheria,” amesema Kamanda Msangi.

Kamanda Msangi ameeleza “Inasemekana kuwa mtoto alikuwa akicheza na watoto wenzake kwenye nyumba anapoishi mtuhumiwa ambayo ipo jirani na nyumbani kwao, ndipo mtuhumiwa alitumia nafasi hiyo ya kuwatuma watoto wenzake kwenda dukani kumnunulia sindano kisha akamchukua mtoto huyo na kumuingiza ndani kwao na kumfanyia ukatili wa kumlawiti uliomsababishia maumivu makali katika sehemu zake za siri.”

 Inadaiwa kuwa baada ya mtuhumiwa kufanya ukatili huo alitoroka na kukikimbilia kusikojulikana, huku akimwacha mtoto akipiga kelele za kuomba msaada ambapo mama wa mtoto alifika kutoa msaada na kumkuta mtoto wake akiwa na hali mbaya ndipo alitoa taarifa kituo cha polisi.

Polisi walikwenda kwa haraka hadi eneo la tukio na kushirikiana na wananchi kumpeleka mtoto hospitali. Mtoto amelazwa hospitali ya wilaya ya ukerewe akiendelea kupatiwa matibabu hali yake inaendelea kuimarika. Msako mkali na ufuatiliaji wa kumtafuta mtuhumiwa wa ukatili huo bado unaendelea.

Kamanda Msangi ametoa wito kwa wakazi wa mkoa wa Mwanza hususani vijana akiwataka kuacha kufanya vitendo vya ukatili kwani ni kosa la jinai. Vilevile amesema vitendo vya ukatili wa aina hii vinapelekea maambukizi ya magonjwa hatarishi hivyo ameoimba jamii kuwa mstari wa mbele kutoa taarifa za watu wenye tabia hizi mapema ili waweze kushughulikiwa.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )