Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Wednesday, July 18, 2018

Muna Love Afunguka Mambo Mazito......Athibitisha Casto ni Baba yake Patrick

adv1
Msanii wa filamu Muna Love leo hii amezungumza na vyombo vya habari  na kueleza kisa kizima cha kifo cha mtoto wake mpendwa marehemu Patrick ambacho kilisababishwa na uvimbe uliojitokeza ghafla kichwani hali iliyopelekea kupoteza maisha pindi akisubiri kufanyiwa upasuaji kuondoa uvimbe huo

Hata hivyo kufutia kifo cha mtoto huyo mambo mengi yaliibuka na kuleta picha tofauti tofauti na maswali mengi.

Moja ya mjadala mzito ulioibuka ni kufahamu nani hasa ni baba mzazi wa mtoto Patrick.

Leo Julai 18, 2018 Muna ameeleza kwa kirefu zaidi na kusema kuwa Casto Dickson ambaye ni mtangazaji wa kipindi cha Clouds maarufu kama Siz Kitaa ndiye baba mzazi wa marehemu Patrick.

Muna amesema kuwa aliolewa na Peter ambaye alidai kuwa ndiye baba mzazi wa Patrick akiwa na ujauzito wa Casto wa wiki mbili ambapo Casto aliukataa, na Peter alikubali kumuoa hivyo hivyo na kulea mimba hiyo.

Aidha amesema ni kweli Peter ni mume wake wa ndoa ambaye wameachana miaka mitano iliyopita na yeye ndiye aliamua kumuacha kufuatia kisa kizito kilichotokea ambacho hakuwa tayari kukiweka wazi, hivyo kwa sasa na tangu kutokea kwa tukio la mtoto kuumwa mpaka kufa Muna na Peter walikuwa wametengana na kila mtu kuwa na maisha yake.

Ametoa shukrani za dhati kabisa kwa watu wote waliojitokeza kumsaidia kumpumzisha mtoto wake kipenzi Patrick.

==>>Zaidi, Msikilize hapo chini
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )