Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Monday, July 16, 2018

Mwanajeshi wa JWTZ Akutwa Amefariki Kisimani

Polisi Mkoa wa Kusini Unguja imesema inaendelea na uchunguzi kubaini sababu za kifo cha askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), ambaye mwili wake ulikutwa kisimani.

Kamanda wa polisi mkoani hapa, Suleiman Hassan Suleiman alisema jana kuwa wanaendelea na uchunguzi, huku akimtaja mwanajeshi huyo kuwa ni Othman Khatib Othman (36), mzaliwa wa kisiwani Pemba.

Suleiman alisema Alhamisi jioni wiki iliyopita, walipata taarifa kutoka kwa wasamaria wema kuwa kuna mwili umeonekana kisimani.

Alisema kisima hicho kipo eneo la Ubago jirani na kambi ya JWTZ alikokuwa akifanya kazi na kwamba, mwili uliopolewa Ijumaa saa 11:45 asubuhi.

Kamanda Suleiman alisema baada ya uchunguzi mwili ulizikwa eneo jirani kutokana na kuharibika, hivyo kushindikana kusafirishwa kupelekwa nyumbani kwao.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )