Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Thursday, July 5, 2018

Nape Kawaonya wanaomzushia kufukuzwa uanachama...."Watapata Tabu Sana Wanuka Maziwa"

Mbunge wa Jimbo la Mtama, Mh. Nape Nnauye amesema kwamba wanaomzushia kwamba amesimamiswa uanachama wa Chama Cha Mapinzduzi watapata tabu sana.

Kauli hiyo ya Nape imekuja baada ya kusambaa taarifa katika mitandao ya kijamii kwamba barua ya Mbunge huyo kusimamishwa uanachama wa Chama chake imekwishamfikia mkononi.

"Kwa uzushi huu watapata tabu sana wanuka maziwa, ndio shida ya kudandia treni kwa mbele, unawakuta wenyeji unakuwa Mwenyezi kuliko" Nape Nnauye.

Mwenyekiti wa CCM ambaye pia ni Rais wa Nchi John Pombe Magufulia mapema wiki hii alionyeshwa kuchukizwa na wabunge wanaotokea mikoa ya Lindi na Mtwara kutokana na michango yao bungeni kwenye suala la korosho ambapo baadhi ya wabunge wa CCM kutokea mikoa hiyo waliitaka serikali iwalipe wakulima pesa ambazo wanadai ili waweze kuendeleza zao hilo.

Hivi karibuni Katibu wa Itikadi, Mawasiliano na Uenezi ACT Wazalendo, Ado Shaibu alidai kwamba hakuna mwanaharakati anayeweza kulitetea Taifa akiwa chini ya Chama tawala hivyo kuwahimiza Nape, Bashe na Hawa Ghasia kuwa kama wana nia ya dhati ya kuwatetea wanyonge wahamie ACT-Wazalendo.


Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )