Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Tuesday, July 3, 2018

Ndege kubwa ATCL kufika mwezi huu

Shirika  la Ndege Tanzania (ATCL) limebainisha kuwa ndege yake mpya yenye uwezo wa kubeba abiria 262, itawasili mwezi huu. Ndege hiyo itafanya safari nchini kwa mwezi mmoja kabla ya kuanza safari zake rasmi kwenda Mumbai, India.

Limesema ikiwa nchini itafanya safari katika viwanja vya Kilimanjaro na Mwanza kwa gharama nafuu, kwa lengo la kuwezesha Watanzania kutumia ndege yao kwa bei ya punguzo.

Mkuu wa Idara ya Biashara, Lily Fungamtama amebainisha hayo katika Maonesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam na kueleza kuwa ndege hiyo ina uwezo wa kwenda safari ya moja kwa moja kwa saa 18 na ya kwanza kwa ajili ya safari za nje ya nchi kwa kuanzia na Mumbai.

Fungamtama amesema, kabla ya mwisho wa mwaka huu, wanatarajia kupokea ndege nyingine mbili hivyo kuongezeka kwa safari za masafa ya mbali.

Amesema, kwa sasa shirika hilo linafanya safari ndani ya nchi katika mikoa ya Kilimanjaro, Mwanza, Mbeya, Tabora, Kigoma, Bukoba na visiwa vya Zanzibar huku wakifanya safari za Songea lakini kwa sasa wamesitisha kwa ajili ya kiwanja kinafanyiwa marekebisho.

Fungamtama amesema kwa nje ya nchi wanafanya safari za Comoro huku wakiwa na mipango ya kuanza safari Bujumbura Burundi na Entebbe Uganda huku wakiwa tayari kukabiliana na ushindani wa kibiashara katika sekta hiyo.

'Hatuogopi ushindani kwani tuko imara katika kuongeza ubora wa huduma zetu, uhakika wa safari, kupunguza kuchelewa, muda, kusitisha safari, pamoja na usalama wa abiria na mali zao, uaminifu, maadili pamoja na kusimamia miongozo ipasavyo,`alisema.

Alisema shirika hilo lina wataalamu waliobobea katika kila sekta kuanzia uongozi hadi huduma ndani ya ndege, kwani wamepikwa na chuo chao na wengine kutoka nje ya nchi huku wakialika watu kusoma katika chuo chao chenye wataalamu waliopitishwa na Mamlaka ya Anga..

“Watanzania wameitikia huduma zetu hasa kwa kuwa na bei shindani, kwa kweli wananchi wanatupa support kubwa pamoja na Rais amekuwa akitusaidia katika kila nyanja hivyo ni vema wananchi kutumia ndege yetu ili kutunza chetu kidumu,`alisema.

Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )