Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Sunday, July 1, 2018

Ofisa Tarafa Atiwa Mbareoni Kwa Kuomba Rushwa ya Laki 3

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoani hapa imemfikisha mahakamani ofisa tarafa ya Siloka katika halmashauri ya wilaya ya Bukombe kwa makosa ya kuomba na kupokea rushwa.

Mshatakiwa huyo Tumbo Madaraka alifikishwa mahakamani mbele ya hakimu wa mahakama ya wilaya ya Bukombe, Veronica Seleman.

Mwendesha mashtaka wa Takukuru, Husna Kiboko aliieleza mahakama kuwa Aprili 28, 2018 katika halmashauri ya wilaya ya Bukombe mshtakiwa  alimkamata mtu aliyebeba magogo bila kibali halali na kumuomba hongo ya Sh350,000 ili asimchukulie hatua za kisheria.

Amedai mahakamani hapo kuwa mshtakiwa huyo alitenda kosa kinyume na kifungu cha 15 cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa namba 11 ya mwaka 2007.

Mshtakiwa alikana kutenda kosa na yuko nje kwa dhamana baada ya kukidhi vigezo vya kuwa na wadhamini wawili wenye mali isiyohamishika yenye thamani ya Sh5 milioni.

Kesi hiyo itatajwa tena Julai 17,2018 kwa ajili ya mshtakiwa kusomewa maelezo ya awali.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )