Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Thursday, July 5, 2018

Ombi hakimu kujitoa kesi vigogo Chadema kujulikana Julai 10

Hatma ya kujitoa ama kutojitoa kwa Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri anayesikiliza kesi ya viongozi 9 wa CHADEMA akiwemo Mwenyekiti Freeman Mbowe kujulikana July 10,2018.

Hatua ya kutaka kujitoa kwa hakimu huyo inatokana na viongozi hao wa CHADEMA kumkataa hakimu huyo kwamba hawana imani naye.

Uamuzi huo wa kujitoa ama kutojitoa, ulitarajiwa kutolewa leo na Hakimu Mashauri baada ya Wakili wa utetezi, Hekima Mwasipu kuieleza  Mahakama kuwa mawakili wenzake  hawapo.

Mwasipu ameeleza kuwa mawakili wanaoiendesha kesi hiyo, Jeremiah Mtobesya na Peter Kibatala hawapo mahakamani kwa sababu  wapo katika  kesi nyingine Mahakama Kuu, pia Paul Kaunda yupo mkoani Shinyanga ambapo pia anaishi.

Naye Wakili wa Serikali Mkuu, Faraja Nchimbi amedai kuwa wamesikia maelezo ya upande wa utetezi na kuongeza kuwa uamuzi huo kutolewa bila ya kuwepo kwa mawakili wa utetezi Kibatala na Mtobesya siyo busara.

Baada ya kusikiliza hoja za pande zote, hakimu Mashauri alikubaliana na Maelezo ya upande wa utetezi na kuiahirisha kesi hadi July 10,2018 ambapo atatoa uamuzi kama ajitoe ama asijitoe.

Mbali na Mbowe, washtakiwa wengine ni Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Vincent Mashinji, Mbunge wa Iringa Mjini Peter Msigwa, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Salum Mwalimu na Naibu katibu Mkuu bara na Mbunge wa Kibamba, John Mnyika.

Pia wengine ni Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche, Mbunge wa Kawe Halima Mdee, Mbunge wa Bunda, Esther Bulaya na Mbunge wa Tarime mjini, Esther Matiko.

Inadaiwa kuwa washtakiwa walitenda makosa hayo February 16, mwaka huu katika maeneo ya Viwanja vya Buibui, Mwananyamala na barabara ya Kawawa Kinondoni Mkwajuni.

Wanadaiwa kuwa Februari 16,mwaka huu katika barabara ya Kawawa Kinondoni Mkwajuni washitakiwa hao wakiwa na wenzao 12 ambao hawapo mahakamani walikiuka tamko la kuwataka kutawanyika la Mrakibu Mwandamizi wa Polisi, Gerald Ngiichi kwa kugoma kutawanyika na kupelekea uvunjifu wa amani.

Inadaiwa kitendo cha kugoma kulisababisha hofu iliyochangia kifo cha Mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwiline na majeruhi kwa askari wawili ambao ni H.7856 PC Fikiri na E.6976 CPL Rahim Msangi.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )