Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Thursday, July 5, 2018

Polisi Dodoma walivyowanasa wahamiaji haramu

adv1
Jeshi la polisi mkoani Dodoma limekamata Wahamiaji haramu 40 Raia wa Ethiopia pamoja na Watanzania wanne waolikuwa wakiwasafirisha Wahamiaji hao.

Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa polisi mkoani hapa Gillis Muroto alisema, Wahamiaji hao walikamatwa katika barabara kuu ya Dodoma kuelekea Arusha kijiji cha Kuhi kata na tarafa ya Bereko Wilayani Kondoa.

Kamanda Muroto Alisema Wahamiaji hao walisafirishwa na gari lenye namba za usajili T. 898 AHM na tela namba T. 422 ADD aina ya Scania mali ya Kampuni ya SANVIC LTD. Watanzania waliokuwa wanawasafirisha Wahamiaji hawa ni Dereva Julius Jackson Kitoma(57) Mnyaturu na mkazi wa Ngarenaro Arusha, Abedi Raphael Nyomolelo (20) Utingo wa gari hilo na Mkazi wa Sakina Arusha.

Wengine ni Ramadhani Salumu Mawazo (39)Mzaramo pia mkulima na mkazi wa Mbagala Dar es Salaam pamoja na Juma Ramadhani Husei (46) Mzigua, mkulima na mkazi wa Kinyerezi Dar es Salaam, aliwataja Muroto.

Aidha alisema kuwa Watuhumiwa hao walitumia mbinu ya kuwafungia Wahamiaji hao kwenye Contena la Mizigo, wakiwachanganya na bidhaa walizokuwa wakizisafirisha ambazo ni maboksi yenye Vizibo vya Soda na bia kutoka Namanga- Arusha kuelekea Mbeya.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )