Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Monday, July 2, 2018

Profesa Mbarawa amshukuru Rais Magufuli kwa kumteua tena

Profesa Makame Mbarawa amemshukuru Rais John Magufuli kwa kumteua tena kuwa waziri, safari hii akipewa Wizara ya Maji na Umwagiliaji.

Katika mabadiliko ya baraza la mawaziri yaliyofanywa na kiongozi mkuu huyo wa nchi jana Jumapili Julai Mosi, 2018, Profesa Mbarawa amehamishwa kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, kwenda wizara yake hiyo mpya.

Mwigulu aenguliwa akiwa mgeni rasmi

Katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter, msomi huyo amemshukuru Rais Magufuli kwa kuendelea kumuamini.

“Namshukuru Rais kwa kuendelea kuniamini na kuniteua tena kwa nafasi ya waziri kuongoza wizara ya maji,” amesema.

“Nawashukuru pia wote ambao tumeendelea kushirikiana katika utumishi kwenye wizara Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano. Tuendelee kushirikiana kwa maendeleo ya Watanzania wote.”
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )