Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Monday, July 23, 2018

Rais John Magufuli na Waziri Mkuu wa Korea Kusini, Lee Nak-Yok Watia Saini Ujenzi wa Daraja la Salender

Rais Dkt. John Magufuli amesema kuwa daraja jipya la Salenda, litakuwa ni ukurasa mpya wa kutengeneza mandhari ya jiji la Dar es salaam kutokana na muonekane wake litapomalizika kujengwa.

Rais Magufuli amesema hayo leo  wakati wa zoezi la utiaji saini kati ya wakala wa barabara  Tanzania (TANROADS) na mkandarasi aliyeshinda zabuni ya ujenzi wa daraja hilo kutoka nchini Korea.

Ujenzi wa daraja hilo eneo la Coco Beach hadi Aga Khan unatarajiwa kufanyika kwa miezi 36.

Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads), Patrick Mfugale amesema mradi huo umelenga kupunguza foleni jijini Dar es Salaam.

Utiaji saini ulishuhudiwa na Rais John Magufuli na Waziri Mkuu wa Korea Kusini, Lee Nak-Yok aliye nchini kwa ziara ya kiserikali.

Mfugale amesema daraja hilo litagharimu Dola milioni 126.26 za Marekani. Amesema Tanzania imechangia asilimia 17.2 na Korea Kusini asilimia 82.2.

Amesema daraja hilo litakuwa na uwezo wa kubeba tani 180 kwa wakati mmoja na magari 55,000 kwa siku moja.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )