Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Wednesday, July 4, 2018

Rais Magufuli akumbushia mbio zake za urais na Lowassa

Rais Dkt. John Magufuli amemsifia Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa kuwa ni mtu mwema sana kwa kile alichokieleza kwamba hakuwahi kumtukana kipindi walichokuwa wanagombea pamoja katika Uchaguzi Mkuu wa Rais wa mwaka 2015.

Dkt. Magufuli ametoa kauli hiyo jana Julai 03, 2018 wakati alipokuwa anazungumza na viongozi wakuu wastaafu aliowaalika kukutana nao katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete Ikulu Jijini Dar es salaam.

"Nilifanya kazi katika kipindi chenu, mzee Mkapa aliniteua kuanzia Naibu Waziri kule ambapo Waziri Mkuu wetu alikuwa mzee Sumaye kwa kipindi chote cha miaka 10. Ikaja awamu ya nne, Waziri Mkuu wetu alikuwa mzee Edward Lowassa na bahati nzuri, uzuri wa Mh. Lowassa wakati wa kampeni tulipokuwa tunagombea wala hakunitukana hata kidogo ni mtu mwema sana huyu", alisema Dkt. Magufuli.

Mbali na hilo, Rais Magufuli amesema kuwa lengo kubwa ya yeye kuwaita wazee hao Ikulu kukaa ni kutaka kuwasalimia kwa kuwa inamuwia vigumu kwenda kwa mmoja mmoja.

"Nimeamua kuwaita hapa ili tukae, tufahamiane, tuzungumze na kama kuna mambo yoyote yale kuzungumza tufanye hivyo na mimi nahitaji busara za wazee ndio sababu kubwa ya kuwaita sina sababu nyingine yoyote lakini pia nimekuwa nimewakumbuka",  alisisitiza Rais Magufuli.

Kwa upande mwingine, Rais Magufuli amesema na yeye anatamani siku moja akiistafu awe miongoni mwa wazee hao.
Advertisement
Loading...
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
==

taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )

Loading...