Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Saturday, July 14, 2018

Rais Magufuli Amwapisha kamishna Mpya wa Magereza jenerali Phaustine Kasike na Kumpa Maagizo Mazito

Rais John Magufuli amemtaka Kamishna Jenerali mpya wa Jeshi la Magereza,  Phaustine Kasike kuchapa kazi kumaliza changamoto zinazolikabili jeshi hilo.

Kiongozi Mkuu huyo wa nchi ametoa kauli hiyo leo Jumamosi Julai 14, 2018 Ikulu jijini Dar es Salaam muda mfupi baada ya kumuapisha kamishna huyo na Balozi Joseph Sokoine ambaye ameteuliwa kuwa naibu katibu mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira).

“Nakupongeza kidogo, lakini pole ndio nyingi,” amesema Rais Magufuli.

Rais Magufuli amemtaka Kasike kuhakikisha wafungwa wanafanya kazi ipasavyo, wazuie matumizi ya simu gerezani, washiriki katika shughuli za kilimo na ujenzi, wazuie kufanya biashara na kushiriki katika matukio ya wizi wakiwa gerezani.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )