Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Monday, July 2, 2018

Rais Magufuli Awataka Viongozi wa Dini Wasiruhusu Siasa Kuingilia Mambo ya Kidini

Viongozi wa dini mbalimbali hapa nchini wametwakiwa  kutoruhusu siasa kuingilia shuguli za dini ili kujenga ustawi wa kanisa na Taifa kwa ujumla pia kutowafanya watu wachche kujinufaisha kupitia taasisi za dini.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Jenista Mhagama  wakati alipomwakilisha Rais Dokta Jihn Pombe Magufuli kwenye misa ya kumweka wakfu Askofu wa sita wa Kanisa la Moraviani Tanzania jimbo la Magharibi.

Mhagama alisema  ni jambo la hatari kwa manufaa na ustawi wa imani pale siasa zitaruhusiwa kuingilia masuala ya dini kwani linaweza likasababisha migawanyiko ambayo sio vizuri kwa maendeleo ya nchi.

Aidha  Mhagama aliwataka  wanasiasa wenzake  kuacha dini zifanye kazi zake bila kuingiliwa na vivyo hivyo siasa zijiendeshe kwa mujibu wa Katiba za vyama kwa kuzingatia Katiba na sheria za nchi.

Alisema  kwamba siasa zikiingilia  dini  zitaleta  migogoro ndani ya dini ambayo  itasabaisha  mifarakano ndani ya taifa na kusababisha  kutoweka kwa amani na utulivu.

Mhagama alisisitiza Serikali itaendelea kushirikiana na na madhehebu ya dini zote kuhakikisha uhuru wa kuabudu unapatikana na kuheshimiwa na Watanzania wote.

Alisema Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dokta John Pombe Magufuli itaendelea kuhakikisha madhehebu mbalimbali ya dini hapa nchini yanaendelea kuendesha shughuli zake bila kubugudhiwa.

 Mhagama alisisitiza  kuwa Serikali haitakubali mtu yoyote anayetaka kusababisha dini zikorofishane ama zigombane na serikali kwani itamchukulia hatua kwa mujibu wa Sheria za Nchi.

 Katika salamu hizo Rais Magufuli alisema anatambua uwepo wa Kanisa la Moraviani katika jitiada zake za kujenga na kuimarisha udugu na kujenga imani na utulivu wa wananchi na ametoa shilingi milioni kumi zisaidie katika kulitegemeza Kanisa na Taasisi zake.

 Awali  askofu mteule wa sita wa kanisa hilo jimbo la Magharibi Ezekiel Yona ameipongeza serikali ya awamu ya tano kwa jinsi inavyoweka mazingira  mazuri ya kuliendeleza kiuchumi taifa la Tanzania.

 Alisema kazi yake ndani ya kanisa hilo itakuwa ni kusisitiza amani, kuhudumia watu kiroho na  kimwili kwa kutoa huduma za kijamiii kwa kushirikiana na serikali.

 Zoezi la kuwekwa wakfu kwa Askofu huyo wa sita limefanyika kwenye viwanja vya kanisa la Moraviani Milumbani mjini Tabora na kusimamiwa na Askofu Dokta Alinikise Cheyo, akisidiana na Maaskofu Conrad Nguvumali na Askofu Sam Gray  toka Amerika.

Viongozi wengine waliohudhuria sherehe hizo ni maaskofu wa kanisa hilo toka majimbo mbali mbalihapa nchini, Mkuu wa Mkoa wa Tabora, wabunge na viongozi wa dini mbalimbali.
Advertisement
Loading...
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
==

taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )

Loading...