Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Thursday, July 26, 2018

Ray C Aguswa na staili ya maisha ya sasa ya Lulu Michael

Msanii mkongwe wa muziki nchini Tanzania, Ray C amejikuta akilengwa na machozi baada ya kuangalia video iliyosambaa mtandaoni ikimuonesha Muigizaji wa Bongo Movie, Elizabeth Michael ‘Lulu’ akicheza kwaya kanisani.

Ray C amedai kuwa video hiyo imemfanya akumbuke kipindi cha nyuma wakati alipopitia kwenye matatizo ya kuugua kwani kipindi hicho alikuwa ni mcha Mungu na alikuwa hakosi kanisani tofauti na sasa.

“Lulu nimeangalia hii video zaid ya mara kumi nahisi!mpaka machozi yamenilenga kwakweli!Sikumbuki lini nimeingia kanisani!“ameandika Ray C kwa kujutia kwenye ukurasa wake wa Instagram na kusisitiza kuwa amejifunza jambo kutoka kwenye video hiyo.

“Najiona mzima sasa na nasahau kuwa Mungu ni mkali! nimejifunza kitu kutoka kwako my dear! kikubwa sana. You Inspire Me..“amemaliza hivyo Ray C.

Picha na video ya Lulu ikimuonesha mwenye afya nzuri akiwa Kanisani akicheza na waumini wenzake ilisambaa Jumatatu ya wiki hii. 

Tazama video yenyewe hapa chini ikimuonesha Lulu akicheza kanisani
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )