Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Sunday, July 1, 2018

RPC Arusha Azungumzia Sakata la Godbless Lema Kushikana Mashati na Polisi

Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema anatarajiwa kesho Julai 2, 2018 kuwasilisha maelezo kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Ramadhani Ng'anzi kuhusu kudhalilishwa hadharani.

Lema anadai kudhalilishwa na mtu anayesadikiwa kuwa ni askari kwa kumshambulia kwa maneno.

Kamanda Ng'anzi amesema  kuwa Lema alimpigia simu akilalamikia kitendo hicho kilichofanyika akiwa saluni na watoto wake wawili.

Amesema tukio hilo lilitokea jana Juni 30, 2018 alipotoka nje kununua skafu ndipo alipokutana na askari huyo anayetajwa kwa jina moja la Anthony.

"Hizi taarifa sijazipata rasmi, nimeziona kwenye mitandao ya kijamii Jumamosi lakini vilevile mbunge alinipigia kulalamikia kitendo alichofanyiwa na kuniahidi kuja kesho tuzungumze suala hilo," amesema Kamanda Ng'anzi.

Amesema wameshafungua jalada na askari wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo kwa kuwa inadaiwa lilifanyika eneo la wazi.

Kamanda Ng’anzi amesema maelezo ya Lema yatasaidia kufahamu chanzo cha mgogoro huo.

Akizungumzia tukio hilo, Lema amedai anafahamiana na askari huyo kwa muda mrefu na amekuwa akitaka amsaidie kukutana na viongozi wake wa juu ili atoe kilio chake cha kushushwa cheo alichokuwa nacho cha Mkaguzi wa Polisi.

Lema amesema hata wakati wa mkutano wa Bunge kuhusu bajeti ya Wizara ya Mambo ya Ndani alitaka kwenda Dodoma ili amsaidie akutane na waziri wa wizara hiyo na Mkuu wa Jeshi la Polisi lakini alimzuia kwa kile alichodai wabunge wa upinzani hawasikilizwi hoja zao.

Mbunge huyo amedai katika hali ya utani alimwomba askari huyo amnunulie skafu, lakini alimrushia maneno ya kashfa ndipo alipomkabili na watu waliokuwa karibu waliingilia kati.

Lema amesema aliamua kurudi saluni ambako askari huyo alimfuata na kuendelea kulalamika kwamba ameshindwa kumsaidia.

Amesema kitendo hicho kilimfadhaisha mbele ya watoto wake na wapiga kura, hivyo ataangalia ni hatua gani za kuchua.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )