Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Thursday, July 12, 2018

Serikali Kufuta Tozo Ya Usajili,kuhuwisha Na Kushikilia Usajili Kwa Wawekezaji Wa Dawa za Wagonjwa Nadra

NA WAMJW-MWANZA
SERIKALI kupitia wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto imefuta tozo ya usajili , kushikilia na kuhuwisha dawa zenye IDADI ndogo ya wagonjwa kwa wawekezaji wote kupitia Mamlaka ya chakula na Dawa (TFDA) .

Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati alipotembelea kuangalia ujenzi wa jengo la (TFDA) ambalo linajengwa Jijini Mwanza ili kusogeza huduma kwa wananchi wa mkoa huo.
 
“Ili kuunga mkono juhudi za Rais Dkt. John Pombe Magufuli za kukuza nchi kupitia uchumi wa viwanda hivyo TFDA msiwe kikwazo kwa wawekezaji hao hivyo kuanzia leo nafuta tozo za kusajili, kushikilia na kuhuwisha dawa (orphan medicines) ambazo zina idadi ndogo ya wagonjwa na magonjwa hayo ni hatarishi ili kuvutia wawekezaji katika eneo hili ”, alisema Waziri Ummy. 

Aidha, Waziri Ummy amewaagiza TFDA kuzipa kipaumbele dawa hizo wakati wa usajili.
 
Aidha Waziri Ummy amesema kuwa kuendana na juhudi hizo pia Serikali imefuta tozo ya udhibiti ya thamani ya 0.25 za dawa,vifaa na vifaa tiba zinazoingizwa kwenye hospitali za Umma kutoka kwa wafadhili.
 
Mbali na hayo Waziri Ummy amesema kuwa TFDA ina wajibu wa kusimamia Tanzania isiwe jalala la bidhaa zisizo na ubora kwa watanzania hivyo wanatakiwa kuweka afya ya wananchi mbele kuliko manufaa binafsi.
 
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TFDA Bi. Agness Kijo amesema kuwa ujenzi wa jengo hilo ukikamilika utasaidia kuhudumia huduma za kimaabara kwa bidhaa zinazoingia nchini kwani itakuwa sio lazima tena kwenda kupima bidhaa hizo jijini Dar es salaam.
 
“Maabara hizi zikikamilika zitasaidia kufanya vipimo na udhibiti wa bidhaa katika mipaka mingi ya Kanda ya Ziwa ikiwemo Sirari, Rusumo na Mutukula ili kuhakiki usalama wa bidhaa zinazoingia nchini kwa lengo la kulinda afya za wananchi.
 
Sambamba na hilo Waziri Ummy alipata nafasi ya kutembelea kukagua ujenzi wa jengo la wodi ya mama na mtoto katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekou toure na kuhakikisha ujenzi unakamilisha ili kuokoa vifo vya mama na mtoto vinavyotokana na uzazi.
 
“Kama watu wa mwanza wanaridhishwa na huduma zinazotolewa katika hospitali hii basi ni lazima huduma za afya ziboreshwe ikiwemo afya ya mama na mtoto hivyo ninaleta mashine ya CT Scan kwa ajili ya kuboresha matibabu hapa” alisema Waziri Ummy.
 
Aidha Waziri Ummy aliwataka watendaji wa Hospitali kutoa taarifa za utendaji kwa Waziri wa Afya na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo pamoja na kusimamiwa na Wakuu wa Mikoa yao ili kuimarisha huduma za afya nchini.
Waziri wa afya,Maendeleo ya jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu kulia  akipata baadhi ya maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Ubora wa Huduma za Afya kutoka Wizara ya afya Dkt. Mohammed Mohammed kushoto wakati alipotembelea kukagua shughuli za ujenzi wa jengo la Mamlaka hiyo jijini Mwanza.
Waziri wa afya,Maendeleo ya jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu kulia akipata maelezo juu ya sukari zinazopimwa ubora wake  kutoka kwa Mkuu wa Maabara wa TFDA Kanda ya Ziwa Bw. Salum Kindoli wakati alipotembelea kukagua shughuli za ujenzi wa jengo la Mamlaka hiyo jijini Mwanza.
Baadhi ya mafundi wakiendelea na shughuli za ujenzi wa wa jengo la wodi    ya mama na mtoto katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekou toure jijini Mwanza- (Picha na Wizara ya Afya)
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )