Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Thursday, July 19, 2018

Twaweza yaijibu Costech kimya kimya

adv1
Mara baada ya kusambaa kwa barua ya Twaweza iliyoandikwa kutokea Costech,Taasisi ya Twaweza imejibu kimya kimya barua waliyoandikiwa na Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Julai 11 2018.

Twaweza imechukua hatua hiyo baada ya kutakiwa na Costech kujieleza kwa nini isichukuliwe hatua za kisheria kwa kosa la kutoa matokeo ya utafiti bila ruhusa.

Meneja utetezi wa taasisi ya Twaweza Annastazia Rugaba amesema kuwa tayari Mkurugenzi Mtendaji wa Twaweza, Aidan Eyakuze ameshajibu barua hiyo tangu Julai 13 na sasa wanasubiri majibu ya Costech.

Julai 11, mwaka huu Costech iliiandikia barua Twaweza na kuitaka kutoa maelezo hayo ikiwa ni siku chache baada ya kutoa ripoti ya utafiti uliopewa jina la ‘Sauti za Wananchi.’

Matokeo ya utafiti huo yalionyesha kuporomoka kwa ukaribu wa wananchi na vyama vya siasa, utekelezaji wa majukumu kwa viongozi walioko madarakani, Rais anavyotekeleza majukumu tangu alipoingia madarakani na uhuru wa kujieleza katika baadhi ya maeneo
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )