Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Monday, July 16, 2018

Ufaransa Bingwa Mpya Kombe La Dunia 2018

Hatimaye kiama cha michuano ya Kombe la Dunia Urusi kimefikia mwisho jana kwa timu ya taifa ya Ufaransa kuweza kutwaa Kombe hilo kwa kuifunga Croatia mabao 4-2.

Mabao ya Ufaransa yaliwekwa kimiani na Mario Mandzukic aliyejifunga, Antoine Griezmann aliyefunga kwa njia ya penati pamoja, Paul Pobga pamoja na Kylian Mpabbe.

Wakati huo mabao ya Croatia yalipachikwa kimiani na Ivan Perisic pamoja na Mario Mandzukic aliyesahihisha makosa yake kwa kuifungia timu yake bao la pili.

Ubingwa huo kwa Ufaransa unakuwa wa pili baada ya kuutwaa pia katika mashindano ya Kombe la Dunia mwaka 1998 nchini kwao.

Kocha wa timu hiyo, Didier Deschamps amekuwa miongoni mwa makocha watatu kutwaa ubingwa huo kama mchezaji na Kocha baada ya Mbrazil Mario Zagallo na Mjerumani Franz Beckenbauer.

Vilevile Ufaransa imekuwa timu ya kwanza kufunga mabao manne katika fainali hizo tangu Brazil iifunge Italia 4-1 mwaka 1970.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )