Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Sunday, July 1, 2018

Urusi Yaing’oa Kwa Matuta Hispania Kombe La Dunia Na Kutinga Robo Fainali

Hatimaye wenyeji wa Kombe la Dunia 2018,  wameendelea kuwafurahisha warusi baada ya kuibandua Hispania, katika michuano ya mwaka huu yanayoendelea kutimua vumbi huko Russia, na kuwafuata Ufaransa na Uruguay katika hatua ya robo fainali.

Katika mchezo wa tatu wa hatua 16, ni vijana wa Fernando Hiero ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao, baada ya beki, Ignashevich, kujifunga mwenyewe, katika juhudi za kuokoa hatari langoni mwao na kufanya idadi ya magoli ya kujifunga katika michuano hii kufika 10 mpaka sasa.

Hata hivyo, wenyeji walifanikiwa kusawazisha bao hilo kwa mkwaju wa penalti na kufanya idadi ya penalti zilizopigwa katika michuano hii kufikia 26 mpaka sasa, baada ya Gerard Pique, kuunawa mpira ndani ya boksi ambapo Artem Dzyuba, alipiga penalti safi na kumpeleka David De Gea marikiti.

Mechi hiyo iliopigwa katika uwanja wa Luzhniki, ilishuhudia dakika 90, zikimalizika kwa sare 1-1. Dakika 30 za nyongeza zikabidi zitumike kutafuta mshindi, lakini bado milango iliendelea kuwa migumu.

Hatua ya matuta ikahusika, kupata mshindi atakayesonga mbele, ikiwa ni kwa mara ya kwanza katika michuano ya mwaka huu. Russia wakaibuka wababe baada ya kukwamisha mikwaju minne dhidi ya mitatu ya Hispania. Mwisho wa siku Russia 5-4 Hispania.

Wapigaji kwa upande wa Spain walikuwa ni Koke (alikosa), Andres Iniesta, Sergio Ramos, Iago Aspas (alikosa) na Gerard Pique. Wapigaji wa Russia ambao wote wakimtungua De Gea ni Alexander Golovin, Ignashevich, Cheryshev na Smolov.

Kwa matokeo hayo, Spain inaungana na Argentina na Portugal kuaga mashindano hayo huku wakiendeleza rekodi mbaya ya kushindwa kuwafunga Wenyeji wa mashindano hata mara moja. Mchezo unaofuata ni kati ya Croatia na Denmark.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )