Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Wednesday, July 4, 2018

Wajapan Wameamua Kumuua Pweza Aliyetabiri Kuhusu mechi ya Japan Kombe la Dunia Huko Urusi

adv1
Pweza anayeaminika kuwa na uwezo wa kipekee, na ambaye alikuwa amefanikiwa kutabiri matokeo ya mechi zote za Japan katika Kombe la Dunia Urusi ameuawa na kuuzwa sokoni awe kitoweo.

Pweza huyo aliyekuwa amepewa jina la Rabio alikuwa amepata sifa si haba baada ya kujaribiwa kwenye kidimbwi kidogo cha watoto na kuwa mtabiri stadi.

Aidha, Kimio Abe, mvuvi aliyemvua kutoka baharini, amesema aliona ni heri kumuuza ageuzwe kuwa chakula badala ya kuendelea kutabiri.

Amesema kuwa alibaini angepata pesa nyingi iwapo angemuuza apikwe na kuwa chakula kitamu cha Kijapani kwa jina sashimi kuliko kama angeendelea kutumiwa kutabiri.

Hata hivyo, Rabio ambaye alikuwa Pweza mkubwa alifanikiwa kubashiri matokeo ya Japan dhidi ya Colombia na pia sare yao dhidi ya Senegal kwa kuhamia maeneo mbalimbali kwenye kidimbwi chake.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )