Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Sunday, July 1, 2018

Waliofariki Katika Ajali Mkoani Mbeya Wafika 20

Watu 20 wamefariki na wengine 45, kujeruhiwa katika ajali iliyohusisha Hiace 3 na Lori lililokuwa limebeba Kontena maeneo ya Mbalizi mkoani Mbeya ambapo kati ya watu hao wanawake ni 12 na wanaume 8.

Kamanda wa Polisi jijini Mbeya Mussa Taibu amesema kuwa chanzo cha ajali hiyo bado hakijajulikana, na uchunguzi unaendelea.

“Ajali hii imehusisha Lori na daladala tatu katika Mlima Iwambi mkaoni hapa na kuzipelekea kudumbukia mtoni , ambapo vifo mpaka sasa ni watu ishirini na majeruhi ni arobaini na tano wamepelekwa katika hospitali ya rufaa ya Mbeya”, amesema Kamanda.

Kamanda ameongeza kuwa jiografia ya eneo hilo imechangia ajali mara kwa mara katika eneo hilo, na kuwasihi madereva kuwa makini na kupunguza mwendo barabarani.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )