Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Thursday, July 12, 2018

Waziri Ummy Mwalimu Amtumbua Dereva wa Gari la Wagonjwa Lililokamatwa na Kilo 800 za Mirungi

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amemuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Tarime, Elias Ntiruhungwa kumsimamisha kazi dereva wa gari la kubeba wagonjwa la halmashauri hiyo aliyekamatwa akiwa amepakia kilo 800 za mirungi.

Kauli hiyo imetolewa leo Alhamisi Julai 12, 2018 katika uzinduzi wa mradi wa Tuwatumikie katika viwanja vya Halmashauri ya Wilaya ya Itilima mkoani Simiyu.

Amesema mbali na dereva huyo, maofisa waliokuwa wamepanda gari hilo nao wasimamishwe kazi.

“Nimesikitishwa na taarifa za kukamatwa kwa gari la kubeba wagonjwa likiwa na mirungi, inasikitisha maana magari yanabadilishwa matumizi huku wagonjwa wakipata shida na wengine hata kufariki dunia,” amesema.

Amewataka waganga wakuu wa wilaya na mikoa kusimamia matumizi ya magari hayo ili wagonjwa wawe wanafika kwa haraka katika vituo vya afya kwa ajili ya matibabu.

Amesisitiza kuwa hataki kuona magari ya wagonjwa yanafanya shughuli nyingine na kuagiza kuwa yanapaswa kuwa katika vituo vya afya yalivyopangiwa.
 
“Ni marufuku gari la kubeba wagonjwa kubeba mkaa wala bidhaa nyingine, nalipongeza jeshi la polisi mkoani Mara kwa kuchukua hatua na mkurugenzi wa mkoa wa Mara nakuagiza kuchukua hatua mara moja usisubiri kusikiliza popote”, amesema ummy.
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )