Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Thursday, July 19, 2018

Ya Kujivunia Katika Infinix Note 5, Teknolojia Ya Android 1 Kamera Na Muonekano Wa Almasi.

Kwa sasa tumekuwa tukiona makampuni ya simu yakizalisha simu mara kwa mara ili kuweza kuongeza idadi ya wateja na kuendelea kuwa kampuni pendwa lakini wanashindwa kuweka utofauti katika simu zao. Kitu ambacho kampuni moja tu ndio imeweza kufauli katika hili kupitia toleo lake jipya la Infinix NOTE 5.

Nikiwa na maana ya kwamba tangu kuanza kwa mwaka huu tumeona kampuni zikizalisha simu za Android 8.1 mpaka imetengeneza mazoea baina ya wanunuaji. Na kwa kupitia huo udhaifu Infinix ndipo walipoleta mapinduzi kupitia infinix NOTE 5 yenye kubeba sifa zake zote katika mfumo wa Android 8.1 ya Android One (A1), ikiwa na maana hata kamera yake inafanyakazi kupitia Android One.
 
Kamera ya Infinix NOTE 5 ni 12MP yenye pixel 1.25um, hivyo basi tunaona Infinix NOTE 5 inauwezo wa kupiga picha nzuri kupitia kamera yake kutokana na pixel ya kamera kuwa kubwa na kamera ya mbele ni 16 iliyo na low light selfie ikiwa na maana hata katika mwanga hafifu bado unaweza kujitwanga selfie na ikakupa picha yenye muonekana mzuri.   
 
Na ili kuifanya simu iwe na muonekana mzuri Infinix NOTE 5 inaumbo jembamba, nyuma ikiwa na muonekana wa kioo kinachong’aa kama alimasi na eneo lake kubwa la mbele limetawaliwa na wigo mpana wa kioo cha 18:9  ya nchi 6.0 FHD (1080*2160) chenye kukufaidisha katika usomaji, uangaliaji movie, kucheza games, kukupa picha yenye uhalisia zaidi lakini pia kugawa kioo cha simu yako na kufanya kazi mbili kwa wakati mmoja ili kuokoa muda lakini pia kioo cha NOTE 5 kinakupa uhuru wakutumia simu yako hata kwenye jua kali. 
 
Na kama jina lake linavyojieleza NOTE 5 ni simu yako wewe mfanyakazi wa ofisini na hata mwanafunzi. Infinix NOTE 5 inastorage kubwa ya GB 32 kwa ram ya GB 3 ni simu yenye uwezo wa kuhifadhi ‘files’ nyingi na kuzitumia kwa wakati mmoja pasipo simu kuelemewa.
 
Ukubwa wa betri yenye ujazo wa 4500mAh, Android One na processor Helio 23 yenye 2.0 Ghz Quard core vyote kwa pamoja vinaifanya simu ya Infinix kuweza kudumu na chaji kwa siku Tatu na zaidi na pasipo masharti katika utumiaji.

Kwa habari nyingi zaidi tembelea tovuti www.infinixmobility.com/tz/ 

Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )