Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Saturday, August 4, 2018

Mgodi Wa Bulyanhulu Hatarini Kufungwa Endapo Watashindwa Kutekeleza Hukumu Ya Mahakama Kuu Shinyanga ya Kulipa Bilioni 3.1

Mahakama  Kuu Kanda ya Shinyanga, imetoa siku saba kwa uongozi wa kampuni ya uchimbaji madini ya dhahabu mgodi wa Bulyanhulu Gold Mine, ulioko Msalala wilayani Kahama, kulipa Sh. bilioni 3.1 inazodaiwa na wafanyakazi 17 ambao waliofukuzwa  kazi.

Naibu Msajili wa Mahakama hiyo, Eugenia Rujwahuka, aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa Mahakama imetoa muda huo kuanzia Julai 31 hadi keshokutwa  fedha hizo ziwe zimeshalipwa. Alisema iweapo kampuni hiyo itashindwa kutekeleza amri hiyo, mahakama itaishikilia akaunti ya mgodi huo.

Alisema kesi hiyo ilifunguliwa na wafanyakazi wa mgodi huo tangu mwaka (2007) kupitia Mahakama Kuu Kanda ya Tabora  na kisha kuhamishiwa Mahakama Kuu Kanda ya Shinyanga miaka 10 iliyopita.

Rujwahuka alisema wametoa muda huo kabla hawajaishikilia akaunti ya mgodi au kusitisha shughuli za uchimbaji wa madini mpaka fedha hizo zitakapolipwa.

"Fedha hizi tumeelekeza zilipwe kwenye akaunti ya Mahakama inayosimamiwa na Benki Kuu ya Tanzania na  sisi tutawapatia wahusika. 

"Mgodi usipofanya hivyo ndani ya siku hizo saba, itatulazimu kuishikilia akaunti yao na kama hakutakuwa na fedha hizo Sh. bilioni 3.1 itabidi tusitishe shughuli zote za mgodi," alisema Rujwahuka.

Aliongeza kuwa: "Nashauri waajiri pale wanapowaachisha kazi wafanyakazi wawe wanawapatia stahiki zao kwa sababu ni haki yao na waachane na tabia ya kuanza kupelekana mahakamani na kuongeza utitiri wa kesi ambazo zingine wangeweza kumalizana wenyewe."

Kesi hiyo ya madai ilifunguliwa na wafanyakazi 1,511 waliokuwa wanafanya kazi ndani ya mgodi huo, lakini baada ya kuchukua muda mrefu kwa kampuni hiyo pale inaposhindwa kukata rufani, ndipo wengine 1,494 wakakata tamaa na kubaki 17 ambao waliifufua na kuendelea nayo.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )