Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Friday, August 10, 2018

Baba Aua Mtoto kwa Kipigo Jijini Mwanza

Mwanafunzi wa kidato cha nne katika Shule ya Sekondari ya Kata ya Sumbugu wilayani Misungwi  jijini Mwanza, Mariamu Tabu (18)amefariki dunia kwa kile kilichodaiwa ni kupigwa na baba yake mzazi baada ya kutohudhuria shuleni.

Akizungumza na wanahabari jana Agosti 9, Kamanda wa Polisi jijini humo Ahmed Msangi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba mtuhumiwa anashikiliwa na polisi kituo cha Misungwi na atafikishwa mahakamani kujibu mashtaka.

Kamanda Msangi amesema kuwa mama mzazi wa Mariam, Kija Mashauri amelieleza Jeshi la Polisi kuwa Agosti 6, mwanaye alikwenda shule lakini hakurudi nyumbani badala yake alirudi Agosti 7 jioni, ndipo baba yake aliuliza alipokuwa na kuanza kumpiga.

“Baba tayari tumemkamata kwa ushirikiano na wananchi, mara baada ya kutekeleza tukio la kumpiga mwanae alitaka kukimbia akazuiwa na wanakijiji, ambapo walimuwahisha mtoto katika zahanati ya kijiji kwakuwa alikuwa katika hali mbaya alifariki akiwa mapokezi”, amesema Msangi.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )