Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Thursday, August 23, 2018

Bobi Wine aachiwa, akamatwa tena na Jeshi la Polisi

Mbunge wa Kyadondo nchini Uganda Robert Kyagulanyi maarufu Bob Wine amekamatwa muda mfupi baada ya mahakama ya kijeshi kumuondolea mashtaka ya umiliki haramu wa silaha nchini humo.

Muda mfupi baada ya kuachiliwa huru, Wine alikamatwa tena na inaarifiwa kwamba anatarajiwa kushtakiwa katika mahakama ya hakimu mkuu kujibu mashtaka ya uhaini pamoja na wabunge wengine waliokamatwa.

Mbunge huyo ambaye pia ni mwanamuziki nchini kwa jina maarufu Bob Wine leo aliwasilishwa katika mahakama ya kijeshi mjini Gulu kaskazini mwa Uganda.

Mawakili wake awali walijuzwa kuwa kesi itasikilizwa katika kambi ya kijeshi ya Makindye anakozuiliwa mjini Kampala.

Mawakili wa jeshi wameeleza mahakama kuwa mashtaka dhidi ya Wine yameondolewa na kwamba mwanasiasa huyo akabidhiwe kwa polisi ili akabiliwe na mashtaka ya uhaini pamoja na wabunge wengine waliokamatwa .
 
Wakili wake Wine Medard Segona ameiambia mahakama kwamba licha ya kuwa wameridhishwa na hatua ya mahakama ya kijeshi , anapinga hatua ya sasa ya mteja wake kuhamishwa katika mahakama ya kiraia kukabiliwa na mashtaka mapya.

Alitaka mbunge huyo aachiwe huru ili aweze kupelekwa kupokea matibabu.

Mahakama iliamua kuwa Bobi Wine yu huru, iwapo hakuna mashtaka mengine yatakayowasilishwa dhidi yake.

Wakati huo Wine alionekana akilia na kupangusa machozi huku hukumu hiyo ikisomwa. Alitoka nje ya mahakama akiwa anatemba kwa magongo na kuonekana kuwa na maumivu makali. Hapo ndipo alipokamatwa upya.

Credit:BBC
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

taboola apo chini
....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )