Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Sunday, August 26, 2018

CHADEMA, ACT Wazalendo Wasusia Uchaguzi wa Marudio Tanga

Vyama vya CHADEMA, ACT Wazalendo na NCCR Mageuzi vimetangaza kugomea kushiriki uchaguzi wa udiwani katika Kata ya Mwanzage jijini Tanga kwa kile walichoeleza ni kuwepo kwa zuio la mahakama juu ya uchaguzi huo.

Wakiongea katika mkutano wa pamoja, viongozi hao wamesema mbali na zuio la mahakama lakini hawaoni kama uchaguzi utakuwa wa huru na haki kutokana na kuwepo kwa mazingira yasiyoridhisha ikiwemo ucheleweshwaji wa kuchukua fomu za kugombea.

''Sababu mama ni zuio la mahakama linaloonesha kufanya uchaguzi ni batili, pili katika uchaguzi uliofanyika kata ya Mabokweni haukuwa wa haki pamoja na matumizi makubwa ya nguvu ya dola', amesema Katibu mkuu wa CHADEMA wilaya ya Tanga Jonathan Baweji.

Naye Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Hamin Kidege ametaja sababu ya chama chao kutoshiriki ni kukosekana kwa uungwana 'Fair play' katika chaguzi za kata mbalimbali zilizopita hivyo hawaoni kama katika kata hii mambo yamebadilika.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi wilaya ya Tanga, Richard Abel amesema chama chake kimeamua kuungana na vyama vingine kujitoa katika uchaguzi huo, kutokana na kupuuzwa kwa agizo la mahakama la kutofanyika kwa uchaguzi huo.

Kwa mujibu wa ratiba ya Tume ya taifa ya uchaguzi (NEC), uchaguzi wa udiwani na wambunge katika kata na majimbo yaliyotangazwa utafanyika Septemba 16, mwaka huu.

Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )