Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Monday, August 20, 2018

Diva Afunguka Kwa Uchungu Kinachomfanya Asipate Mtoto

Mtangazaji wa kipindi cha Ala za Roho kutoka Clouds FM, Diva amefungukaa kile ambacho kinapelekea yeye kutobeba ujauzito.

Diva ambaye pia anafanya muziki wa Bongo Fleva ametumia ukurasa wake wa Instagram kueleza changamoto kubwa anayopitia kwa sasa anapohitaji kupata mtoto. 

==>>Tazama hapo chini kusoma alichokiandika Diva.
Nitachokiandika ni kitu ambacho kinaumiza sana Moyo wangu , Naandika Machozi yakiwa yananitoka , Sikutaka kuandika lakini Nahitaji kuandika ili nipate msaada zaidi, Sababu haya ni maisha yangu na naandika toka moyoni sitajali mtu atanifikiria nini au atawaza nini, hii situation is confusing sana na ndio maana nimeshindwa hata kulala yan nashindwa kulala kwa ajili ya hii issue sio tu kulala hata kula vizuri siwezi , Moyo wangu una maumivu mengi sana.

Nimejiuliza maswali sipati, ila nimeamua kuandika hapa, Kwa muda sasa kama mwaka niliamua kutafuta mtoto, Nimekunywa kila aina ya dawa mnayoijua nyinyi, za hospitali ndio nimemeza mpaka ikafika kipindi nikachoka, hizo za kunywa ndio nimemeza mpaka nimechoka, nikaamua kuchukua likizo kwa ajili ya vipimo very deep kujua tatizo ni nini, In my life nishawahi kupata ujauzito lakini haukufika ata Miezi4 and i lost the baby, kiukweli ilivyotokea mimi mwenyewe nilishang'aa, ila kwa ajili ya mambo yaliyokuwa yanaendelea kwenye hio relationship na huyo mwanaume anaitwa Solomoni frank.

Niliona labda Mungu ana Mipango yake, too many lies, so i decided to step out n focus on me ,how i met him Sitaki hata kuandika hapa ila iko siku i will share , Hivyo Basi nikakutana na Madaktari wa TMJ hospital nikafanya kipimo kujua kwanini kupata ujauzito inakuwa mtihani sana. sababu vipimo vyote vilikuwa sawa nikaamua kufanya kipimo cha mirija, ambacho nilifanya 9th july 2018.

Kwa Mtu alieniona hii siku atagundua nilikuwa na maumivu sana , Nililia sana sijawahi lia kama hivyo katika maisha yangu, Nililia sana Nilikuwa na maumivu sina mfano wa kuyafananisha, went to see Dr, Msemo wa Sanitas hosp ambae pia anafanya kazi TMJ ili nijue hasa tatizo , Yeye ni Daktari wangu , Akaniambia majibu yapo umekutwa na Bilateral Cornual Block yaani mirija imeziba, ata kupata mtoto kwa njia ya kawaida inakuwa maajabu sana. alivyokuwa ananielezea.

 Nilijikuta nalia Machozi yana teremka, nilishindwa drive i was in deep pain, nilitamani yule mtoto aliepotea arudi. at some point Sikuwa Pia naamini Mungu ana Exist, historia tu ya maisha yangu ilinifanya nitamani sana mtoto wangu mwenyewe afu the moment nahitaji sana ndio napewa haya majibu.

Basi nilijikuta nalia kupita maelezo ....had to call a friend called @qqtrends4u and gladly she was there for me wakati huu wote alikuwa yeye na @soudybrown ndio walini comfort 😭😭 i was heartbroken , tumeambiwa friends to keep ... hao ndio my friends to keep .. i love them sana sijui hata nieleze vipi hakuna maneno sahihi ya kueleza.

Mungu Mkali sana Nilisema, Mimi Diva ambae natoa misaada , nasaidia, moyo wangu una utu imekuaje haya mambo yanitokee nilijiuliza sana ... sikuweza kulala wala kula mpaka nililazwa kwa kupata Presha, but Nikaanza kuomba kwa Mungu Nikasema hii ni mara ya mwisho naomba.

Nikampigia doctor isaac nikamueleza akaniambia Gods Timing.... mambo yatakuwa sawa, nimeamua kuongea labda kuna wanawake pia wanapitia hii situation , ni situation inaumiza sana na kila ninapokutana na swali utazaa lini nakuwa naumia na hili swali sababu yan mimi Diva hata abortion sifanyi why on earth this imetokea.

wakati wa ukuaji wangu nimeumwa sana na tumbo na naumwa sana na tumbo, nishawahi fanyiwa upasuaji, hivyo solution ilikuwa kuwa na mtoto ili tatizo la maumivu makali ya tumbo kuisha, hivyo naweza sema nimepitia machungu mengi in my life but stil leo usiku huu nimeamka na kuamua kuandika hivi nimemuomba sana Mungu nikasema Im going public with this.

Bila aibu wala uoga na ntasaidia wengine pia wapate msaada ninaohitaji mimi wakati huu sababu najua maumivu yake, naandika hii part 2 chozi au niseme machozi yananitoka. Everything happens for a reason right, i have my best friend called @iammelissa_1 nilikuwa nae kwa simu kwa muda akasema Diva Najua unachopitia, "I know it’s a sensitive subject and sad for you to talk about!

But maybe you should talk about it because you are a great influence in your country and have many fans that are maybe having the same trouble as you So you could help them too talking about it " hivyo nikakaa chini na kuamua kuandika Hivi ninavyoandika .. i believe God is real ... nikaamua kufungua a page ntaweka link on inaitwa Gofundme.com na kuanzisha Kampeni inaitwa ' Dreams , Hopes , Wishes . Nia is to have a donation ya $7000 kwa ajili ya ivf treatment in America. Namshukuru Daktari wangu alisema haya....

Mayai na kizazi chako vyote viko sawa , but unaweza fanya IVF treatment #ivfjourney nikaamua kuwatafuta madaktari wa nje ya nchi kujua nafanyaje, with the amount of money sababu kuna kuishi huko, kula, kwa siku kadhaa pamoja na kupata sperm donor hivyo hio amount inaweza kutosha.

Guys ntaweka link hapo from gofundme , ili kama unaweza uchangie sababu mimi hizo hela sina siwezi danganya, thats alot of money, hivyo link apo juu wil help to support My Campaign called ' Dreams, Hopes, Wishes so that i can have My Miracle Baby baby of my own ....

Nahangaika kupata mtoto sasa hivi sababu ndio umri sahihi, sitaki sema how much nafanya kazi , nalala 2 hours too, nikisikia sauti ya yule daktari kichwani au ndotoni naamka usingizi unaisha unakata, imagine nimebeba all this moyoni mwezi mzima uliopita , Natembea na maumivu ya Majibu ya Daktari, ila nashukuru amenieleza vizuri tu Daktari wangu amesema ' Diva Your stil young , you can have it all done just pray , save for the treatment , keep calm n collected ... have faith ....

Yan wakati wengine wanapata watoto wanatupa, some of us needs alot of money for this treatment , dahhh 😭😭😭😭imagine i even set a baby name , baby room, i so wanted in my life mwaka huu niwe na mtoto 1 tu a baby boy afu mambo yanatokea so fast then huja recover unapata all the news za blockage ..... kumbe zinasumbua sana .. na upasuaji wake nao ni kazi ingine to deal with, kipimo chake tu ni maumivu sijawahi pata ona . ila Nimeandika sababu It is completely sensitive I know but you can imagine the pain i feel everyday.

The Pain ambayo wanawake wengine wanapitia, ni ngumu sana .. moyo ni kiza kinene msione mtu anacheka, wanawake tunapitia majaribu mengi sana i dont kno why!... nacheka, nafanya kazi , spend time with my family n friends ... nafanya mambo mengine lakini Moyo wangu umevunjika ... Sina raha ...

 Niko kwenye huzuni kubwa sana maishani... Naamini Mungu yupo na anasikia kilio changu Maana Nimelia sana mpaka nimechoka nimesali sana πŸ™ hivyo Pia naomba Mniombee sana ... thanksπŸ’• love you all πŸ™ or you can send the money - Diva Gissele AC/ 3007111473924 Equity Bank, link on bio for Money transfer πŸ™
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

taboola apo chini
....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )