Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Monday, August 6, 2018

Diwani Mwingine wa CHADEMA Kahamia CCM

Madiwani wawili wa Chadema na NCCR-Mageuzi  manispaa ya Bukoba wamejiuzulu uanachama na kujiunga na CCM, Akiwemo meya wa zamani wa manispaa hiyo, Dk Anatory Aman.

Dk Aman  aliyekuwa diwani wa Kagondo Agosti 20, 2015 alihama CCM na kujiunga na NCCR-Mageuzi na kuwania udiwani katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 25, 2015.

Mbali na Dk Aman, mwingine ni aliyekuwa diwani wa Hamugembe (Chadema), Muhaji Kachwamba. Wote wameshakabidhi  barua za kujivua nyadhifa zao katika ofisi za CCM Mkoa wa Kagera tukio lililoshuhudiwa na viongozi mbalimbali.

Akitaja sababu za kurejea CCM, Dk Aman amesema ameridhishwa na utendaji kazi wa Rais John Magufuli.

Amesema CCM ni sehemu sahihi ambayo anaweza kumsaidia Rais Magufuli kutekeleza ilani ya chama hicho tawala, kubainisha kuwa ameondoka NCCR na waliokuwa wakimuunga mkono.

Mwenyekiti wa CCM manispaa ya Bukoba, Ioas Muganyizi amesema milango bado ipo wazi kwa wanachama wengine wanaotaka kujiunga na chama hicho.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )