Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Saturday, August 11, 2018

Hakimu aionya Jamhuri kesi ya vigogo wa Simba

adv1
Mahakama  ya Hakimu Mkazi Kisutu imetoa siku saba  hadi Agosti 7 kwa upande wa Jamhuri kukamilisha mchakato wa kubadilisha hati ya mashtaka ili kuwaondoa washtakiwa wawili katika kesi inayomkabili aliyekua Rais wa  klabu ya Simba, Evans Aveva na makamu wake, Godfrey Nyange (Kaburu).

Washtakiwa wanaotakiwa kuondolewa katika kesi hiyo ni Zacharia Hanspope na Frank Lauwo ambao hawajawahi kufika mahakamani hapo.

Mapema, mahakama hiyo ilikubali upande wa Jamhuri kubadilisha hati ya mashtaka kutoka washtakiwa wawili na kuwaunganisha Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya klabu hiyo, Zacharia Hans Poppe na mfanyabiashara Franklin Lauwo.

Hati hiyo, ilisomwa katika mahakama hiyo iliyoketi chini ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba na upande wa Jamhuri ulidai kuwa upelelezi umekamilika.

Hata hivyo, Wakili wa Serikali Leonard Swai alidai kesi hiyo haiwezi kuanza kusikilizwa kwa sababu washtakiwa wawili bado hawajakamatwa.

Upande wa utetezi, ulipinga na uliomba hati ya mashtaka kufanyiwa mabadiliko kwa kuwaondoa washtakiwa ambao hawajakamatwa ili Aveva na Kaburu wajue hatima yao na mahakama iliamuru hati kubadilishwa.

Jana, Jamhuri ulidai kuwa wanasubiri kibali cha DPP cha kuwaondoa washtakiwa wawili ili kuwasomea maelezo ya awali marais hao.

"Mheshimiwa hakimu DPP bado yuko nje ya Dar es Salaam tunaahidi kwamba hata kama yuko Dodoma tutamfuata au hapa hapa Dar es Salaam ili akamilishe hatua ya kuruhusu kesi hii kuendelea," alidai Swai.

Mara baada ya kudai hayo, mshtakiwa wa kwanza, Aveva  aliiomba mahakama hiyo kupanga tarehe za karibu ili waweze kusikiliza kesi hiyo kwa madai kuwa imechukua muda mrefu huku wakili wa Jamhuri, Shadrack Kimaro na wa Takukuru, Swai wamekuwa wakirushiana mpira.

Mshtakiwa wa pili, Kaburu amedai kuwa ni zaidi ya mwaka mmoja sasa umepita wapo mahabusu tangu kesi hiyo ianze kusikilizwa mahakamani hapo huku mawakili hao wakidai faili lipo kwa DPP.

Alidai mshtakiwa wa kwanza, Aveva ana matatizo ya kiafya na kwamba kila wiki anaenda kliniki kwa ajili ya matibabu hivyo kuendelea kurushiana mpira ni kuwaumiza.

Alidai hadhani kwamba si DPP ameshindwa kushughulikia kesi yao, bali ni ucheweshaji wa makusudi unaofanywa na mawakili hao katika kesi hiyo kutoka kwa DPP na Takukuru.

Alidai upelelezi umeshakamilika kilichobaki ni kubadilisha hati hiyo ili kesi ianze kusikilizwa, hivyo aliiomba mahakama hiyo kupanga tarehe za karibuni ili waweze kuwaona na kuwaonea huruma kuliko kupanga tarehe za mbali.

Wakili Swai alidai kuwa hoja zilizotolewa na washtakiwa hao zina mashiko na kuahidi kushughulikia suala hilo.

Hata hivyo, Hakimu Simba alitoa siku saba kwa upande wa Jamhuri kukamilisha mchakato wa kubadilisha hati ya mashtaka ili kesi hiyo iweze kusikilizwa.

“Ukiangalia afya ya Aveva unaona kabisa ni mgonjwa, anatakiwa kwenda kliniki kwa wiki mara mbili, hivyo basi tunalazimika kuangalia ratiba ya matibabu yake ili tupange kesi,” alisema Hakimu Simba.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )