Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Wednesday, August 15, 2018

Hamisa Mobetto na Zamaradi Ndani Ya Bifu Zito

Mtangazaji na mfanyabiashara Zamaradi Mketema ameingia ndani ya bifu zito na Mzazi mwenza wa Diamond Platnumz Hamisa Mobetto Kwenye mitandao ya kijamii.

Kisa cha majibizano hayo ni baada ya kuwepo kwa tuhuma za Zamaradi kuiba idea ya mshono wa nguo yake aliyovaa Kwenye 40 ya mtoto wake kutoka kwa Hamisa Mobetto kisha kwenda kushona kwa fundi mwingine bila hata taarifa.

Baada ya tetesi hizo Zamaradi aliandika Kwenye ukurasa wake wa Instagram kuwa hakuchukua idea ya mshono kutoka kwa Hamisa  bali yeye ndiye alimpa Hamisa mshono lakini alishindwa kushona kwake kutokana na muda.

"Nimeambiwa nilipewa mshono na mtu nikaenda kushona kwingine, na nimeshangazwa na uongo mkubwa wa namna hii, Mimi ndio nimetuma mshono kwake na sio yeye, hakuwa anaufahamu kabla, kutokana na kudai kupishana na muda nikaamua nikashone kwingine na zaidi swala la kushona kokote ni uamuzi wangu since sijachukua mshono wa mtu”. Aliandika Zamaradu

Baada ya povu hilo la Zamaradi, Hamisa na yeye alimwaga povu zito sana na kuandika haya kupitia ukurasa wake wa Instagram huku akiwa ameambatanisha message walivyokuwa wanachat:
 
"First Of All Me sio Mtu wa Kujibishana Na watu insta Ndo maana always nakaaga Kimya ....... Tangia Nimefungua @mobettostyles Kila siku imekua Jipya .

"Secondly sijawahi Sema Popote kuhusu mshono Wa Shughuli yako wala kuandika kwa My page so probably one of your friends kayapeleka sehemu .


"My dear ulivyokua hujanialika kwenye shughuli yako nilibezwa kuchekwa kutukanwa and all siku jibu wala ongea popote kwasababu kila mtu ana uhuru wa kuchagua watu atakao .

"Ulinitafta Tumechagua Mishono umeenda shona kwengine sijawah lalamika my dear wala kusikitika Coz ridhki mafungu saba na kila likuepukalo najuaga huwa lina kheri na Mtu .

"Hivyo basi kama mtu mzima ungeskia kitu ungenifata na kunambia lakin no umeamua kunichafua just because uweze lala vizuri usiku .

#MniacheJamani#MaanaNadhanSikuMkinitoaRoho #MtafurahiaSana "
tangazo
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )