Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Monday, August 27, 2018

Hatima ya Nondo Kujulikana leo Mahakamani

Mahakama ya Wilaya ya Iringa  leo inatarajia kutoa mwongozo wa kesi ya Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP), Abdul Nondo kama atakuwa na kesi ya kujibu au la baada ya upande wa mashitaka kuhitimisha ushahidi wao.

Nondo anakabiliwa na mashtaka mawili likiwamo la kuchapisha taarifa za uongo mtandaoni Machi 7, mwaka huu akiwa eneo la Ubungo, Dar es Salaam na kuzisambaza kupitia mtandao wa kijamii wa Whatsapp kwamba yupo hatarini.

Katika shtaka la pili, anadaiwa kutoa taarifa za uongo kwa mtumishi wa umma Mafinga alipokuwa anatoa taarifa kwa askari kwenye Kituo cha Polisi Mafinga kwa kusema kuwa alitekwa na watu wasiojulikana Dar es Salaam na kupelekwa Kiwanda cha Pareto Mafinga.

Katika kesi hiyo Nondo anatetewa na mawakili wawili wakiongozwa na Jebra Kambole chini ya mtandao wa watetezi wa haki za binadamu nchini (THRDC).
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )