Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Wednesday, August 22, 2018

Idadi ya Wagonjwa waliopandikizwa Figo Hospitali ya Taifa Muhimbili yafikia 19

Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) inaendelea kutoa huduma ya kupandikiza figo ambapo hadi hivi sasa tayari wagonjwa 19 wamenufaika na huduma hiyo tangu ilipoanzishwa kwa mara ya kwanza hapa nchini  Novemba mwaka 2017.

Utoaji wa huduma hiyo ni utekelezaji wa azma ya Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ambayo ili elekeza kuweka mipango thabiti ya kupunguza rufaa za wagonjwa kwenda nje ya nchi kwa ajili ya matibabu ambayo yalikuwa hayatolewi hapa nchini ama kutokana na wataalam wa kutoa huduma hizo au vifaa vya uchunguzi.

Taarifa hiyo imetolewa  jana na Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Hospitali ya Taifa Muhimbili Dkt. Hedwiga Swai alipokua akizungumza na waandishi wa habari kwa niaba ya Prof. Lawrence Museru kuhusu  upandikizaji figo.

“Tunapenda kuwafahamisha kuwa wagonjwa wote tuliowapandikiza figo pamoja na ndugu zao waliojitolea figo wanaendelea vizuri na shughuli zao kama kawaida. Hii inaonesha ni kwa kiwango gani huduma hii imefanikiwa tangu ilipoanzishwa Novemba mwaka jana ”. alisema Dkt Swai.

Akifafanua alisema zoezi hilo la upandikizaji  figo limeshirikisha wataalamu wazalendo toka Hospitali ya Taifa Muhimbili, Hospitali ya BLK, Taasisi ya Saifee iliyopo Mumbai India pamoja na Hospitali ya kimataifa ya Sakra ya nchini India.

“Tunapenda kuwataarifu kuwa katika kutoa huduma hii, tayari wataalamu wetu wa ndani hususani Madaktari bingwa wa upasuaji wamepata ujuzi wa kufanya upandikizaji wenyewe kwa kiwango cha asilimia 75 huku asilimia 25 wakielekezwa na wataalamu kutoka nje. 

"Hii ni hatua kubwa sana katika kuongeza ujuzi wa kutoa huduma hiyo. Maeneo mengine tayari wamefikia asilimia 100 hususani wauguzi wa vyumba vya upasuaji, Madaktari bingwa wa tiba ya magonjwa ya figo (Nephrologists), wataalam wa vipimo vya maabara na Radiolojia."

Kwa mujibu wa Dkt. Swai MNH  itaendelea kufanya upasuaji kwa wagonjwa watano kila mwezi ikiwa ni mpango  wa muda mfupi katika kipindi cha mwaka mmoja na nusu kuanzia sasa ambapo mpango wa muda mrefu  ni kufanya upasuaji kwa mgonjwa mmoja kila siku sawa na wagonjwa 20 kwa mwezi ambapo watakuwa wagonjwa 200 hadi 240 kwa mwaka.

Kwa upande wake Daktari bingwa wa magonjwa ya figo Hospitali ya Taifa Muhimbili Onesmo Kisanga alisema utafiti uliofanyika Kaskazini mwa Tanzania unaonesha kwamba asilimia 6.8 wana matatizo ya ugonjwa wa figo. 

Hivyo amewashauri Watanzania kupima afya zao angalau mara moja kwa mwaka na kuepuka matumizi mabaya ya dawa bila ushauri wa Daktari ili kuepuka magonjwa hayo.

Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

taboola apo chini
....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )