Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Friday, August 3, 2018

Jeshi La Polisi La Kamata Wahalifu 96 Na Silaha Mbili Katika Operesheni.

Mkuu wa Operesheni Maalum za Jeshi la Polisi, Naibu Kamishna Liberates Sabas amesema Jeshi la Polisi kwa sasa linaendesha Operesheni mkoani Mtwara kwa kushirikiana na Nchi ya Msumbiji ili kuwakabili wahalifu wanaokimbili nchini humu

Aidha  Jeshi la Polisi kupitia Operesheni Maalum inayoendelea mkoani Mtwara limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa 96 kati yao 10 wamefikishwa mahakamani kwa kesi mbalimbali na  wengine 16 wamefikishwa katika idara ya Uhamiaji kwa makosa yanayohusu maswala ya uhamiaji, katika operesheni hiyo kumepatikana silaha mbili zilizokuwa zikitumiwa na wahalifu katika maeneo mbalimbali.

Aidha Afande Sabas amewashukuru wananchi wa Mkoa wa Mtwara kwa kuendelea kutoa ushirikiano mzuri ndani ya Jeshi la Polisi na kuwataka wananchi wote nchini kuendelea kutoa ushirikiano ili kutokomeza uhalifu nchini.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )