Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Tuesday, August 21, 2018

Kamati Ya Bunge Yakaribisha Wadau Kutoa Maoni Mbalimbali Kuhusu Miswada ya Sheria

Katika kutekeleza Masharti ya Kanuni ya 84 (2) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la Januari, 2016 kuhusiana na umuhimu wa maoni ya Wadau katika mchakato wa uchambuzi wa Miswada ya Sheria katika ngazi ya Kamati za Bunge, Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ndugu Stephen Kagaigai anautangazia Umma kwamba, Kamati za Bunge zitafanya zoezi la kukusanya maoni ya Wadau mbalimbali kuhusiana na Miswada ifuatayo ya Sheria -:
  1.     Kamati ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii, ) itapokea maoni ya Wadau kuhusu Muswada wa Bodi ya Kitaalam ya Walimu (The Teachers’ Professional Board Bill, 2018 siku ya Alhamisi tarehe 23 Agosti, 2018
  2.     Kamati ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa, ) itapokea maoni ya Wadau kuhusu Muswada wa Sheria ya Tamko la kutangaza Jiji la Dodoma kuwa Makao Makuu ya Nchi wa Mwaka 2018 [The Dodoma Capita City (Declaration) Bill, 2018] siku ya Alhamisi tarehe 23 Agosti, 2018
  3.     Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria, ) itapokea maoni ya Wadau kuhusu Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na.2 ) wa Mwaka 2018 [The Written Laws (Miscellaneous Amendments) (No.2) Bill, 2018]  na Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali  (Na.2 ) wa Mwaka 2018 [The Written Laws (Miscellaneous Amendments) (No.3) Bill, 2018] siku ya Ijumaa tarehe 24 Agosti, 2018
  4.     Kamati ya Bunge ya Bajeti itapokea maoni ya Wadau kuhusu Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi wa Mwaka 2018 [The Public Private Partnership (Amendment) Bill, 2018 siku ya Jumatatu tarehe 27 na siku ya Jumanne tarehe 28, Agosti, 2018.
Kwa Tangazo hili, Wadau mbalimbali mnakaribishwa kwa ajili ya kutoa maoni yenu kwenye Kumbi zilizopo Jengo la Msekwa na Jengo la Utawala katika Viwanja vya Bunge Mjini Dodoma katika kuaniza saa 3 asubuhi.

Sheria zilizotajwa zinaweza kupakuliwa (downloadable) katika tovuti ya Bunge la Tanzania (www.parliament.go.tz). Aidha, maoni ya Wadau yanaweza pia kuwasilishwa kwa barua pepe kupitia cna@bunge.go.tz au njia ya posta kwa anuani ifuatayo:

Katibu wa Bunge
Ofisi ya Bunge
S.L.P 941
DODOMA

Imetolewa na:    Kitengo cha Habari, Elimu kwa Umma na Mawasiliano
Ofisi ya Bunge
DODOMA
21 Agosti, 2018.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )