Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Friday, August 3, 2018

Katibu Mkuu Hazina Awafunda Mameja Wa TRA Nchini

Serikali  imeiagiza Mamlaka ya Mapato nchini (TRA), kuhakikisha inakuwa na uhusiano mwema na walipakodi ili kuondoka dhana iliyojengeka kuwa mamlaka hiyo inatumia nguvu na vitisho katika kudai kodi.

Agizo hilo lilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dotto James, wakati wa mkutano wa maofisa wa TRA wa nchini.

"Mchukue hatua za makusudi kuboresha uhusiano kati yenu na walipa kodi ili kuondoa dhana iliyojengeka kuwa Mamlaka ya Mapato TRA inatumia nguvu na vitisho katika kudai kodi, " alisema James.

James alisema majadiliano ni jambo muhimu katika kujenga uhusiano bora wa kufanya biashara na kuimarisha ulipaji kodi kwa hiyari.

Akifafanua alisema Sh. trilioni 20.15 ni mapato ya ndani kutoka Serikali Kuu na Sh. trilioni 18 yanayotokana na kodi ambayo inatakiwa ikusanywe na TRA.

Alisema wizara, idara, taasisi na mashirika ya Umma, yanatarajia kukusanya Sh. trilioni 2.15.

Alisema katika mwaka huu wa fedha 2018/2019 sera ya mapato inalenga kuongeza wigo wa kodi, kuimarisha usimamizi wa vyanzo vilivyopo hususani katika matumizi ya mfumo wa kieletroniki na hatua nyingine za kiutawala.

Alisema kuwa serikali inaendelea na uunganishaji wa wizara, Idara, wakala, taasisi na mashirika ya umma kwenye mfumo wa serikali wa kieletroniki wa ukusanyaji mapato ili kuboresha ukusanyaji na udhibiti wa upotevu wa mapato ya serikali.

Aidha, alisema madhumuni ya mkutano huo ni kujadili namna ya utekelezaji wa bajeti ya serikali ya mwaka 2018/2019 pamoja na kuweka mipango madhubuti ya namna ya kufikia malengo hayo.

Alisema mkutano huo pia unatoa fursa kwa washiriki wote wanaohusika katika ukusanyaji wa kodi kujadili changamoto mbalimbali zilizopo na kuzitafutia ufumbuzi kwa lengo la kuimarisha ukusanyaji wa mapato na kufikia lengo la mwaka huu la Sh. trilioni 18 ifikapo Juni mwaka 2019.

"Matumaini yangu ni kwamba tutafikia malengo na kuvuka kwa kuwa masuala mengi ya kisera na utendaji yatajitokeza kwenye majadiliano yetu," alisema James.

Wajumbe wa Menejimenti wa Wizara ya Fedha na Mipango, wakiwa pamoja na Viongozi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA, kujadili namna ya kuhakikisha kuwa zaidi ya shilingi trilioni 18 kati ya shilingi trilioni 32.47 zilizopitishwa na Bunge kwa ajili ya Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2018/2019 zinazotakiwa kukusanywa na Mamlaka hiyo zinapatikana kwa ajili ya kugharamia miradi mbalimbali ya maendeleo.

Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )