Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Sunday, August 19, 2018

Magari Matano Ya Mizigo Yatekeketea Kwa Moto Boda Ya Rusumo Mkoani Kagera

Magari matano ya mizigo yameteketea kwa moto katika kituo cha forodha Rusumo Wilaya ya Ngara mkoani Kagera mpakani mwa Tanzania na Rwanda baada ya gari la mafuta ya petrol kuligonga gari jingine na kupoteza mfumo wa breki.

Kamanda wa polisi mkoani Kagera Augustino Olomi amethibisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa yuko njiani akielekea eneo la tukio na taarifa zaidi itatolewa kuhusiana na kiasi cha mali iliyoungua.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Ngara, Luteni Kanali Michael amesema ukosefu wa zimamoto ni changamoto kubwa wilayani Ngara kutokana na matukio ya ajali ya moto kuongezeka na ombi lilishatumwa serikalini lakini utekelezaji wake haujafiki.

Ikumbukwe Julai 6, katika mkutano wake na waandishi wa habari Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola aliwashusha vyeo makamanda wawili kwakushindwa kudhibiti ajali, ambao ni Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Mbeya pamoja na Kamanda wa Kikosi cha Zimamoto Mkoa wa Kagera ambapo alidai kuwa wameshindwa kutekeleza majukumu yao.

Julai 24, 2018 akiwa jijini Arusha Waziri Lugola alitoa onyo kwa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kuacha mara moja tabia ya kutokwenda kwenye matukio ya moto kwa kisingizio cha kutokuwa na vifaa vya kutosha.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )