Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Monday, August 6, 2018

Mawakili wa CHADEMA Kibatala na Mtobesya waikwamisha Kesi ya Akina Mbowe

adv1
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imehairisha Kesi inayowakabili viongozi wa ngazi za juu na Wabunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) leo, hadi Agosti 13, 2018 kwa kile kilichodaiwa kutofika kwa mawakili wanaosimamia kesi yao.

Maamuzi hayo yametolewa na Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Wilbard Mashauri leo Agosti 06, 2018 baada ya kutolewa udhuru wa kutokuwepo Mahakamani hapo kwa mawakili wa upande wa utetezi, Peter Kibatala na Jeremiah Mtobesya kutokana na mawakili hao kuwa na kesi nyingine wanazifuatilia.

Akiwakilisha udhuru huo kwa niaba yao, Wakili wa upande wa utetezi Hekima Mwasipu aliiambia Mahakama kuwa Wakili Kibatala yupo Mahakama Kuu mbele ya Jaji Luvanda ambako alikuwa na shauri jingine, huku Wakili Mtobesya naye pia ana kesi nyingine Mahakama Kuu Mtwara.

Mbali na hilo, Hakimu Mashauri amemuonya mshtakiwa namba 5 ambaye ni Mbunge wa Tarime vijijini kutorudia kuondoka bila kutoa taarifa sahihi kwa mdhamini wake, kwa kuwa ilielezwa mahakamani hapo amekwenda nchini Kenya.

Mnamo Agosti 02, 2018 mshtakiwa huyo alishindwa kuhudhuria Mahakamani kama alivyotakiwa kwa kile alichokieleza Mahakamani hapo leo, kuwa alipigiwa simu ya dharula na mwalimu anayemfundisha mtoto wake akimtaka aende shuleni hapo kwa kuwa mwanae anaumwa.

Usikilizwaji wa kesi ya CHADEMA umekuwa ukihairishwa mara kwa mara kutokana na baadhi ya washtakiwa kutoka ndani ya chama hicho kushindwa kufika Mahakamani kusikiliza kesi, kutokana na dharula wanazozipata pamoja na Mawakili wao pia kuwepo katika Mahakama nyingine wakiendelea na kesi.

Viongozi wa CHADEMA wanaoshtakiwa ni pamoja na Mwenyekiti wao Freeman Mbowe, Katibu Mkuu wa chama hicho Dkt. Vicent Mashinji, Naibu Katibu Mkuu bara John Mnyika, Naibu katibu Mkuu Zanzibar, Salim Mwalimu.

Wengine ni Mbunge wa Tarime vijijini John Heche, Mbunge Tarime mjini Esther Matiko, Mbunge wa Bunda mjini Ester Bulaya, Mbunge wa Iringa Mjini Peter Msigwa pamoja na Mbunge wa Kawe Halima Mdee.

Wote hao wanaandamwa na mashtaka 13 ikiwemo la kufanya mkusanyiko isiyokuwa na kibali kwenye chaguzi ndogo za marudio Jimbo la Kinondoni Jijini Dar es Salaam zilizofanyika Februari 17, 2018
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )