Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Sunday, August 26, 2018

Mbosso afunguka kumuimbia Diamond baada ya kuachwa na Zari

Msanii wa muziki Bongo, Mbosso amesema si kweli kwamba wimbo wake unaokwenda kwa jina la Nimekuzoea alimuimbia Diamond Platnumz baada ya kuachwa na mzazi mwenzie, Zari The Bosslady.

Muimbaji huyo kutokea WCB katika mahojiano na The Playlist ya Times FM amesema wimbo huo ulikutana na tukio hilo na ulikuwepo kwa kipindi kirefu.

"Hapana, ni wimbo ambao ulikutana tu na tukio, ni wimbo wangu ambao nilishawahi kuimba zamani sana kipindi nipo Yamoto Band," amesema.

"Sasa nilipokuja kuingia WCB ni moja ya nyimbo zangu alikuwa anazipenda sana Bosi (Diamond), akaniambi inabidi uufanye, sasa kipindi ambacho nautoa ndio ua mwana  wa weusi," amesema Mbosso.

Wimbo wa Mbosso, Nimekuzoea ulitoka February 09, 2018 wakati usiku wa February 14, 2018 ambayo ilikuwa ni siku ya Wapendanao (Valentine Day) ndipo Zari The Bosslady aliposti Ua Jeusi kwenye ukurasa wake wa Instagram na kueleza kuwa ameachana rasmi na Diamond Platnumz.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

taboola apo chini
....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )